Flatnews

Zitto Kabwe ataka mshinidi aapishwe Zanzibar

Mbunge mteule wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya Chama Cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe amefunguka na kusema kuwa matokeo ya uchaguzi wa Zan...


Mbunge mteule wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya Chama Cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe amefunguka na kusema kuwa matokeo ya uchaguzi wa Zanzibar yatangazwe na mshindi aapishwe.



Zitto Kabwe amesema hayo kupitia ukurasa wake wa Facebook na kudai kuwa suala la Zanzibar lisidharauliwe kabisa kwani hawawezi kutazama Katiba ikikanyagwa,vinginevyo amesema Maalim Seif apate Jaji amwapishe na aunde Serikali mara moja.

"Suala la Zanzibar lisidharauliwe kabisa. Matokeo yatangazwe na mshindi aapishwe. Hatuwezi kutazama tu Katiba inakanyagwa. Vinginevyo Maalim Seif apate Jaji amwapishe na aunde Serikali mara moja na kuanza kuwatumikia Wazanzibari, Serikali ya Umoja wa kitaifa kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar" Amesema Zitto Kabwe
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha.Mnamo tarehe 28 Oktoba alitangaza kufuta matokeo ya Uchaguzi Zanzibar, uliofanyika Oktoba 25, 2015. Jecha alisema kuwa, ZEC imefuta matokeo ya uchaguzi kutokana na kukiukwa kwa sheria na taratibu mbalimbali za uchaguzi wakati wa utekelezaji wa zoezi hilo.Na kutangaza Uchaguzi huo kurudiwa.

Related

NEWS 8997475485829585549

Post a Comment

emo-but-icon

item