Flatnews

Barnaba - sasa naenda Kimataifa

Msanii Barnaba amesema kitendo cha yeye kufanya kazi na msanii mkubwa nchini Uganda Jose Chameleone, ni moja ya viashiria ...


Msanii Barnaba amesema kitendo cha yeye kufanya kazi na msanii mkubwa nchini Uganda Jose Chameleone, ni moja ya viashiria kuwa sasa ameanza kupiga hatua kwenda kimataifa.
Barbana ameyasema hayo kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, na kusema kwamba yeye ni msanii mzuri hivyo ni lazima afanane na thamani ya muziki wake.

"Kufanya Kazi na Jose Chameleone inamaanisha kwamba Barnaba ameanza kutoa mguu wake kwenye soko la Kitanzania na kuvusha muziki wake na kuelekea kwenye safari ya International, lakini pia kuongeza thamani ya muziki wa Barnaba na kuongeza mashabiki wengine wapya kwenye nchi tofauti tofauti, ukizingatia Barnaba ni mwanamuziki mzuri, ni lazima nitengeneze credit na nifanane na ile value ambayo watu wananitunuku", alisema Barnaba.
Barnaba aliendelea kusema kwamba ili afike mbali ni lazima atafute wasanii wakubwa waliofika katika masoko ya kimataifa ili wamsaidie kumpa nguvu
"So lazima nitafute watu wakubwa amabao wameendelea kwenye masoko ya international wanisaidie kupush na kunisogeza kwenye sehemu ambazo huenda nimewahi kufika kidogo au sijawahi kufika", alisema Barnaba.
Pia Barnaba ametolea ufafanuzi suala la kutotengeneza cd yenye cover ya Josee, na kueleza kwamba amefanya hivyo kwa sababu za kibiashara.
"Nimefanya makusudi kwasababu nataka kutengeneza rotation ya kupata pesa, music it's a business and this is my business, kwa hivyo niligundua suala la kutengeneza CD linafanya watu wengi kupata wimbo kirahisi, mwisho wa siku wanashindwa kwenda kwenye zile mitandao ambazo sisi tunakwenda kusell zile nyimbo zetu, so marketing inakuwa ndogo", alisema Barnaba.

Related

ENTERTAINMENT 8602901070372185363

Post a Comment

emo-but-icon

item