Flatnews

Serikali yashauriwa kutoa elimu wakaguzi wa ndani

Serikali imeshauriwa kutoa elimu zaidi kwa wakaguzi wa ndani na wa nje juu ya mfumo wa kieletroniki ili kuwawezesha kufanya kazi za...


Serikali imeshauriwa kutoa elimu zaidi kwa wakaguzi wa ndani na wa nje juu ya mfumo wa kieletroniki ili kuwawezesha kufanya kazi zao kisasa na kitaalamu zaidi.


Mkurugenzi wa utawala na rasilimali watu kutoka ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali ,Gerald Mwanilwa
hayo yameelezwa na baadhi ya wakaguzi waliofanya vizuri katika mitihani yao, na kutangazwa kuwa machampioni wa kuwafundisha wenzao, ambao wamehimiza matumizi ya mfumo wa kieletroniki katika ukaguzi kuwa ni mzuri na huchukua muda mfupi katika ufanyaji kazi sambamba na kuondoa matumizi ya karatasi yasiyo ya lazima .
Aidha Wakaguzi hao wamekiri kuwa bado kuna changamoto ya uelewa wa matumizi ya mfumo huo hivyo kuishauri serikali kuendelea kutoa mafunzo zaidi ili kuongeza uelewa na urahisi wa ufanyaji wa kazi..
Kuwa Upande wake Mkurugenzi wa utawala na rasilimali watu kutoka ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali ,Gerald Mwanilwa,pamoja na kuhimiza uwajibikaji kwa wakaguzi,amesema mfumo huo mpya wa kiukaguzi utasaidia kuokoa rasilimali za nchi na kuahidi ofisi hiyo kushirikiana na ofisi ya Taifa ya ukaguzi kuhakikisha matumizi ya taifa yanàtumika vizuri.

Related

NEWS 1520991360938760471

Post a Comment

emo-but-icon

item