Flatnews

Siri nzito yatawala Mazungumzo ya Maalim Seif na Dk.Shein

Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein na Makamu wake, Maalim Seif Shari...



Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein na Makamu wake, Maalim Seif Sharif Hama.
Siri nzito imetawala  katika mkutano wa Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein aliyekuwa mgombea wa nafasi ya urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamad aliyekuwa mgombea wa Chama cha Wananchi (CUF).

Kwa mujibu wa taarifa za uhakika  zimebainisha kuwa kwamba viongozi hao walikutana kwa mara ya kwanza tangu kumalizika kwa uchaguzi ulioacha utata visiwani chini ya mazungumzo yaliyohudhuriwa na viongozi wakuu wastaafu ambao ni wazee wanaoheshimika
Hadi leo  Ikulu ya Zanzibar haijawa tayari kusema lolote kuhusu mazungumzo hayo ambayo yamekuwa yakisubiriwa kwa hamu na wananchi wa Zanzibar kwa lengo la kujua mustakabali wa kisiasa na kumaliza joto la kisiasa visiwani humo.
Mmoja wa Ofisa wa Ikulu alithibitisha na kukiri kuwepo kwa mazungumzo hayo baada ya kuuona msafara wa Makamu wa Kwanza wa Rais ukiingia Ikulu, lakini hakuwa tayari kufafanua zaidi.
<a href='https://mpakasi.com/ads/www/delivery/ck.php?n=a08724c9&cb=Math.random()' target='_blank'><img src='https://mpakasi.com/ads/www/delivery/avw.php?zoneid=19&source=https%3A%2F%2Fmpakasi.com&cb=Math.random()&n=a08724c9' border='0' alt='' /></a>
Naye Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi hivi karibuni  alieleza kuwa  serikali itawachukulia hatua wote waliovuruga uchaguzi huo, huku CUF wakilalamika na kupinga maamuzi ya ZEC.
Kwa upande mwingine Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salim Jecha ame endelea kulalamikiwa kwa uamuzi wa wake wa kufuta uchaguzi mkuu visiwani humo.

Related

NEWS 9164897266733473327

Post a Comment

emo-but-icon

item