Rais wa Uganda MH,Yoweri Museveni aingia studio tena
Rais wa Uganda, Mheshimiwa Yoweri Museveni ametenga muda wake na kuingia studio kuandaa rekodi inayosimama kwa jina Kwezi,...
https://samchardtz.blogspot.com/2015/11/rais-wa-uganda-mhyoweri-museveni-aingia.html
Rais wa Uganda, Mheshimiwa Yoweri Museveni
ametenga muda wake na kuingia studio kuandaa rekodi inayosimama kwa jina
Kwezi, ikiwa inaeleweka wazi kuwa hatua hiyo ni kwa ajili ya mbio za
uchaguzi mkuu wa nchi hiyo mapema mwaka ujao.
Kazi
hiyo ambayo imekwishakamilika inabeba mashairi ya mheshimiwa akiwa
anazungumzia chama chake tawala cha NRM na mafanikio ambayo ameyapata
katika uongozi wake, tayari kabisa kwa kuingia mtaani kuburudisha
mashabiki na kumuongezea idadi ya wapiga kura hususan wale wapenzi wa
muziki wake.
Rekodi hii ya Rais Museveni inakuwa ni ya pili kutoka, ikiwa imetayarishwa kwa ushirikiano na producer Washington ambaye alipata nafasi ya mualiko maalum Ikulu kwa ajili ya kutengeneza na kurekodi mdundo huo mpya wa Museveni.