Flatnews

MENEJA WA SHIRIKA LA BIMA YA TAIFA KANDA YA KATI DODOMA Bw.ANTONI SINTATONI ALIPO TEMBELEA KITUO CHA WATOTO WENYE ULEMAVU MLALI WILAYANI KONGWA MKOANI DODOMA.

     Watanzania  wametakiwa kujenga utamaduni wa kutoa misaada na kuwasaidia watu wenye mahitaji maalumu ili nao waweze kujikwamua n...




 
   Watanzania  wametakiwa kujenga utamaduni wa kutoa misaada na kuwasaidia watu wenye mahitaji maalumu ili nao waweze kujikwamua na hali ngumu ya maisha..

Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa shirika la BIMA ya taifa kanda ya kati  Dodoma bwana Antoni Sintatoni alipotembelea kituo cha watoto wenye ulemavu wa viungo kilichopo Mlali wilayani Kongwa mkoani Dodoma.
Amesema shirika la bima mkoani dodoma  limemsaidia mama Priska mkazi wa dodoma ambaye ana mtoto mwenye ulemavu wa viungo kwa kumpatia baiskeli ya kutembelea na kuchukua jukumu  la kumpatia mahitaji ya dawa ambapo shirika hilo limempatia  kiasi cha shilingi laki tano  kwa ajili ya manunuzi ya dawa,mafuta na sabuni.


Kwa upande wake mkurugenzi wa kituo hicho kinachomilikiwa na shirika la Fransisco Wakapuchini Padre Paul Sherio amesema kituo hicho kinakabiliwa na changamoto lukuki ikiwemo uhaba wa fedha,mishahara midogo kwa wafanyakazi na baadhi ya wazazi wanaowatelekeza watoto wao.
NA MWANDISHI WETU PRISCA MASSAWE DODOMA

Related

NEWS 1853247557118090429

Post a Comment

emo-but-icon

item