Flatnews

MKURUGENZI WA SHULE YA DAR MUSLIMEEN ILIOKO MJINI DODOMA Bw,MUSLIM YUSUPHU AMETOA MSAADA WA MADAWATI 54 KTK SHULE YA MLIMWA C,LEO.

                           BW.MUSLIM YUSUPH AKIWAONYESHA MADAWATI HAYO KWA KWAKUU WA SHULE HIYO.


                          
BW.MUSLIM YUSUPH AKIWAONYESHA MADAWATI HAYO KWA KWAKUU WA SHULE HIYO.

                    BW.MUSLIM YUSUPH AKIKABIDHI MSAADA HUO WA MADAWATI.
 MAKAMU MKURUGENZI AKIPOKEA MADAWATI HAYO.
 
 Shule ya msingi mlimwa ‘C’ imepokea msaada wa madawati 54 kutoka kwa meneja wa shule ya dar- ur-muslim  bwana Muslim Yusuph Husein ambaye ameguswa na changamoto  ya upungufu wa madawati katika shule hiyo.
Msaada huo wa madawati  umekabidhiwa  leo katika shule hiyo ya mlimwa  c iliyopo katika kata  ya miyuji  na kupokelewa na  mgeni rasmi   Bwana Valentino  Gange  mkurugenzi msaidizi wa tamisemi kwa  kushilikiana na   mwalimu mkuu,walimu wote wa shule,wanafunzi pamoja na wazazi.
Akitoa shukrani zake kwa mfadhili huyo Mkuu wa shule ya msingi ya Mlimwa b Bibi  Magret Elibaliki amemshukuru mkurugenzi wa shule ya dar-ur-muslim kwa moyo wake  wa majitoleo  hususani katika Nyanja ya elimu.
Aidha Bibi  Elibariki  amesema kuwa japo wamepata msaada huo wa madawati lakini bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa maji safi na salama ,vyumba vya madarasa, ofisi ya walimu,viti na meza za walimu,nyumba za walimu,bendera ya taifa ,matundu ya vyoo vya wanafunzi  ambavyo havikidhi  mahitaji na upungufu wa madawati 165.
Mgeni rasmi Bwana Valentino Gange ametoa shukrani zake za dhati kwa bwana Yusuph kuwa ameonesha moyo wa dhati na wa mfano wa kuigwa katika jamii na kuwataka wanajamii wengine kuiga mfano wake.

NA MWANDISHI WETU/WINNIE FRANCIS/ DODOMA





Related

NEWS 4396646610927891777

Post a Comment

emo-but-icon

item