Flatnews

BAADA YA KUFANYA VYEMA TP MAZEMBE, KUNA KILA DALILI SAMATTA AKATIMKIA UFARANSA

Wakati Rais wa TP Mazembe akiwa ameshamuwashia Samatta taa ya kijani tayari kuelekea barani Ulaya kucheza soka la kulipwa, kuna taarifa ...


Wakati Rais wa TP Mazembe akiwa ameshamuwashia Samatta taa ya kijani tayari kuelekea barani Ulaya kucheza soka la kulipwa, kuna taarifa zinasema nyota huyo tayari ameshapata klabu ambayo inashiriki ligi kuu nchini Ufaransa (Ligue 1) na iko tayari kumchukua Samatta kwenda kukipiga kwenye klabu hiyo.

Klabu ya Lille inatajwa kuwa moja ya vilabu ambavyo vinamuwania kwa karibu Mbwana Samatta. Meneja wa Samatta Jamal Kasongo amethibitisha kuwa mchezaji wake atatimkia Ufaransa lakini amekataa kuitaja timu ambayo atajiunga nayo.
“Nisingependa sana kuitaja timu, lakini Moise Katumbi ni mtu mwenye nguvu sana kwa Mbwana kwasababu ameishi naye vizuri na nafasi hii ya Ufaransa yeye mwenyewe Katumbi ndiye anayehusika”, amesema Kasongo.
“Tunashindwa kuitaja timu kwasababu hatujafungua bado hiyo ofa ikoje kwasababu bado iko mfukoni kwa Katumbi, mimi na Mbwana mwenyewe hiyo taarifa tumeshapewa na ni kweli hiyo timu nimetajiwa ni suala la kuwa wavumilivu. Timu ya Lille ndiyo imeonesha interest kubwa kwa Mbwana lakini hatuwezi kusema anakwenda hapo kwasababu ofa zipo nyingi sana”.
“Moise Katumbi ameniambia tayari kuna timu Ufaransa ipo tayari kumchukua Mbwana na kila kitu kipo sawa kwahiyo kilicho mbele sasahivi ni kuweza kuona Samatta anakwenda wapi angalau sasa kunamashindano mengine makubwa yamekuja baada ya kushinda ubingwa wa Afrika, mashindano ya vilabu bingwa duniani ambayo yatafanyika Japan mwezi December”.
“Mashindano haya ni muhimu kwasababu Barcelona na timu nyingine zitakuwepo kwahiyo ni muhimu kwake yeye kufanya vizuri ili kumpa thamani zaidi ya kuweza kucheza Ulaya na timu kubwa kuweza kumtambua na kumuwekea mikakati”.
“Lakini tumeona Ufaransa ni mahali pazuri kwa yeye kuanza kucheza licha ya kwamba kulikuwepo maeneo menine ambako angeweza kucheza kutokana na aina yake ya mpira, mfano kama Hispania, au Ubelgiji lakini Ubelgiji ni ligi ndogo lakini kipaumbele kwetu ilikuwa ni Ufaransa”.

Related

SPORTS 2095218258475778463

Post a Comment

emo-but-icon

item