Flatnews

HICHI NDICHO ALICHOKISEMA MH,ZITTO KABWE KUHUSIANA NA WIZARA YA MICHEZO...BOFYA HAPO CHINI USOME ALICHO KIONGEA>>>

Kiongozi mkuu wa chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe ameshauri kwamba, wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. John Magufuli ...


Kiongozi mkuu wa chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe ameshauri kwamba, wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. John Magufuli atakapokuwa akitangaza baraza lake la mawaziri, aipe nafasi kubwa sekta ya michezo na burudani na itapendeza endapo itapewa wizara yake inayojitegemea na sio kuirundika kwenye sekta nyingine ili kutoa nafasi kwa sekta hiyo kufanya kazi vizvuri kwasababu itakuwa ikijitegemea.

Zitto pia amemshauri Magufuli amteuwe waziri atakayekuwa makini ambaye ataweza kufanya kazi yake kwa ufanisi zaidi huku akiongeza kuwa ni vyema kama Wizara hiyo itakuwa chini ya ofisi ya Waziri Mkuu.
Jana kituo cha Clouds FM kupitia kipindi chake cha Sports Extra kilifnya mahojiano maalum na Zitto ambaye amekuwa ni mdau mkubwa wa masuala ya michezo na burudani nchini kutaka kujua mtazamo na ushauri  wake kwa Rais kuhusu masuala ya michezo hasa kipindi hiki ambacho watanzania wanasubiri kusikia baraza la mawaziri ambao watafanya kazi bega kwa bega na Rais Magufuli likitangazwa.
Sports Etra: Katika kipindi hiki ambacho tunasubiri kusikia baraza la mawaziri likitangazwa, nini mtazamo wako na ushauri kwa Rais Magufuli kuhusu masuala ya michezo ikiwa ni pamoja na mtu wa aina gani ateuliwe kushika wizara inayohusu masuala ya michezo?
Zitto: Michezo na burudani tayari ni sekta nyeti ya uchumi na tayari kwa mara ya kwanza katika taarifa za kiserikali za uchumi, mwaka huu waziri wa fedha aliweka sekta ya burudani kama moja ya sekta rasmi kwenye uchumi wetu na kuonesha kwamba inachangia takribani shilingi za kitanzania bilioni 240 kwa mwaka.
Kwahiyo tayari sekta hii imeshakuwa rasmi lakini pili sekta hii inaajiri watu wengi sana kuliko viwanda vingi sana hata tungejenga viwanda vya namna gani. Kwa mapendekezo yangu, tunatakiwa kuwa tuwe na muono tofauti, yale mambo ya kuchanganya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo tuyaache, michezo na burudani tuipe Wizara yake pekeyake.
Nimeona watu wameanza kusambaza taarifa za baraza jipya la mawaziri litakavyokuwa wameunganisha humo mpaka na ajira, ni watu ambao wanashindwa kuona mambo kwenye mapana yake. Hatuna uhakika kama Rais Magufuli ni mpenda michezo au hapana, mimi sijawahi kumuona uwanjani hata sikumoja hasa kwenye mpira wa miguu.
Lakini kwa vyovyote vile kwasababu yeye ni Rais wa watanzania wote ni vizuri sana ajaribu kuona kama kunauwezekano tuwe na Wizara ambayo inahusika na na michezo na burudani tu. Na siyo lazima iwe Wizara kamili kama ambavyo imekuwa kwenye Wizara kamili nyingine, kutokana na umuhimu wa michezo kuna umuhimu wa kurasmisha sekta hii, kunahaja kama ndani ya ofisi ya Waziri Mkuu kukawa na Waziri wa nchi ambaye anahusika na michezo, utamaduni na burudani.
Hiyo itafanya tuwe na serikali ambayo inaonesha kabisa kuna mtu akilala akiamka yeye anawaza michezo, anawaza Taifa Stars, Bongo Movies, Bongo Flavor, na kila shughuli za kiutamaduni na michezo. Na ikiwa chini ya ofisi ya Waziri Mkuu itakuwa na heshima yakena haitaleta maneno ya kuongezwa ukubwa wa serikali kwasababu atakuwa ni waziri wa nchi ndani ya ofisi ya Waziri Mkuu, kwa maana nyingine atakaye kuwa waziri wa michezo ni yeye mwenye Waziri Mkuu.
Sports Extra: Serikali ya awamu ya nne ilijitahidi sana kuwekeza katika michezo japo bado hayajaonekana matokeo ya moja kwa moja, Je, Mh. Magufuli akitengeneza Wizara kama uliyoipendekeza unadhani itakuwa suluhisho la michezo na burudani kwa upande wa nchi yetu?
Zitto: Tatizo kubwa la michezo kwetu ni kutokuwekeza, sisi watanzania tunataka mafanikio bila kuyagharamia. Hatuwezi kuwa na timu nzuri ya taifa ya mpira wa miguu kama hatuna shule za kukuza vipaji vya vijana ambao wanacheza mpira wa miguu, na sio shule moja au mbili.
Niliwahi kusema huko nyuma mwaka 2006 baada ya matokeo mabovu ya Ujerumani, maana walikuwa waandaji wa mashindano ya kombe la dunia mwaka huo lakini waliishia nafasi ya tatu. Ujerumani iliamua kuwa na program ya miaka 10 ya kujenga vijana ambao watachukua ubingwa wa kombe la dunia.
Tuliwaona wakichukua ubingwa mwaka 2014 na kuifunga Brazil magoli saba kwasababu kila mji ulihakikisha una chuo na serikali ikagharamia na kuhakikisha vijana wanakusanywa na vipaji vinapatikana.
Sasa hapa Tanzania tunataka tuwe na mafanikio bila ya kuwa na uwekezaji, unapokuwa na Wizara inayohusika moja kwa moja na michezo na burudani, maana yake ni lazima tufanye uwekezaji wa kutosha. Kuna hatua imeshapigwa sasahivi chini ya Rais Kikwete hatua inayofuata sasa ni kuwekeza vya kutosha kuhakikisha kwamba huu mchango kwenye pato la taifa unaongezeka, tunatengeneza ajira za kutosha kwa vijana wetu na kujenga heshima ya nchi.
Kwasababu kuna watu wanadhani ukiwekeza kwenye michezo unapoteza pesa, hapana, kwamfano timu yako ya riadha ikienda kwenye michezo ya Common Wealth ikachukua medali za dhahabu maana yake ni kwamba umeitangaza nchi, timu ya mpira wa kikapu ikienda ikafanya vizuri mkatoa wachezaji wazuri kwenda nje umeitangaza nchi.
Juzi mchezaji mmoja tu wa Tanzania Mbwana Samatta ameitangaza nchi dunia nzima wakati wa mchezo wa fainali kati ya timu yake ya TP Mazembe dhidi ya USM Alger kwa kuwa mfungaji bora, sasa pata picha tungekuwa na wachezaji kama yeye wengi wapo kwenye vilabu vingi.
Kunahaja kubwa sana ya Rais kuhakikisha tunwekeza vya kutosha, tufumbe macho tuwekeze kila mkoa uwe na Academy iendeshwe vizuri tuhakikishe kwamba kila timu ambayo ipo ligi kuu moja ya sifa iwe na academy ili tuweze kuzalisha wanamichezo wa kutosha kwa fani zote na siyo mpira wa miguu pekeyake.
Kwahiyo kuwa na Wizara haitoshi, ni lazima pia tuwekeze ili tuweze kuhakikisha kwamba tunapiga hatua kwenye sekta ya michezo.

Related

SPORTS 8372934280911899373

Post a Comment

emo-but-icon

item