Bilal mgeni rasmi sherehe za Idd leo
BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) limetangaza kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya sherehe za Idd El Hajj leo yanayof...
https://samchardtz.blogspot.com/2015/09/bilal-mgeni-rasmi-sherehe-za-idd-leo.html

Bakwata
ilieleza jana kuwa sherehe hizo zitafanyika katika mji wa Musoma na Idd
itaswaliwa kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Mkendo, saa mbili asubuhi
na Baraza la Idd saa nane mchana.
Sikukuu
ya Idd el Hajj au Idd el-Adha inaadhimishwa baada ya kukamilika kwa
ibada ya Hija, moja ya nguzo tano za dini ya Kiislamu ambapo kwa sasa
mahujaji wako katika ibada hiyo nchini Saudi Arabia.
Mjini
Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali
Mohamed Shein anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Baraza la Idd,
litakalofanyika Mkokotoni mkoa wa Kaskazini Unguja.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na Waziri wa Katiba na Sheria wa
Zanzibar, Abubakar Khamis Bakary, swala ya Idd inatazamiwa kufanyika
kitaifa katika Msikiti wa Mkokotoni na Baraza la Idd kufanyika katika
Chuo cha Amali, Mkokotoni Unguja.
“Maandalizi
ya swala ya Eid na Baraza la Eid yamekamilika ambapo kitaifa utafanyika
katika Mkoa wa Kaskazini Unguja, Mkokotoni,” alisema Bakary.