BARCA YATULIZWA LA LIGA, YAPOKEA KIPIGO CHA MBWA MWIZI
Barcelona wamechpwa bao 4-1 na Celta Vigo kwa mara ya kwanza msimu huu kwenye mechi za ligi ya Hispania marufu kama La Liga mchezo ...
https://samchardtz.blogspot.com/2015/09/barca-yatulizwa-la-liga-yapokea-kipigo.html
Barcelona
wamechpwa bao 4-1 na Celta Vigo kwa mara ya kwanza msimu huu kwenye
mechi za ligi ya Hispania marufu kama La Liga mchezo uliochezwa Jumatano
usiku.
Nalito alianza kuifunga timu yake
ya zamani na kuipa Celta Vigo bao la kuongoza huku akimtengenezea Iago
Aspas mabao mengine mawili kwenye mchezo ambao safu ya ulinzi ya
Barcelona inayoongozwa na Gerard Pique ikionekana kuyumba.
Shuti la Lionel Messi liligonga
mwamba mapema mwa kipindi cha pili huku mlinda mlango wa Celta Vigo
Sergio Alvarez akiokoa michomo kadhaa kabla hajafungwa na Neymar wakati
wenyeji Celta wakikamilisha ushindi wao wa goli 4-1 kwa goli la dakika
za lala salama lililofungwa na John Guidetti aliyeingia akitokea benchi.
Ushindi huo kwa Celta unawafanya
wafikishe pointi 13 kwa mechi tano ambazo wamecheza hadi sasa katika
msimu huu wakati kichapo hicho kwa upande wa Barcelona kinakuwa ni cha
kwanza kufuatia kuanza ligi vyema kwa ushindi wa michezo minne
iliyopita.
Celta walianza vyema mchezo huo
lakini Barcelona walitengeneza nafasi dakiza za mwazo za kipindi cha
kwanza. Iniesta alikimbia na mpira kabla ya kumuwekea Messi pasi murua
lakini shuti lake liliokolewa na golikipa wa Celta Sergio Alvarez.
