ARSENAL YAITWANGA TOTTENHAM NA KUSONGA MBELE CAPITAL ONE
Timu ya Arsenal imeshinda 2-1 kwenye mechi ya Capital One dhidi ya mahasimu wao wa jiji la London Kaskazini Tottenham mechi iliyoch...
https://samchardtz.blogspot.com/2015/09/arsenal-yaitwanga-tottenham-na-kusonga.html
Timu
ya Arsenal imeshinda 2-1 kwenye mechi ya Capital One dhidi ya mahasimu
wao wa jiji la London Kaskazini Tottenham mechi iliyochezwa Jumatano
usiku kwenye dimba la White Hart Lane na kutinga hatua ya raundi ya nne
ya michuano ya hiyo ya Capital One.
Mathieu Flamini alikuwa shujaa wa
mchezo huo akipiga goli zote mbili za Arsenal, Flamini alianza kupiga
goli la kwanza dakika ya 26 kipindi cha kwanza na goli hilo kudumu hadi
kipindi cha kwanza kinamalizika.
Calum Chambers alijifunga kuwapa
Tottenham goli la kusawazisha dakika ya 56 lakini goli la dakika ya 78
lililofungwa na Flamini lilitosha kuwapa Arsena ushindi wa London Derby.
