Msaidizi wa Naibu Katibu Mkuu CCM Bara ajiunga Chadema
Bw. Jumanne Juma Msunga. Na Hillary Shoo, SINGIDA MSAIDIZI wa Naibu Katibu Mkuu wa (CCM) Bara, Jumanne Juma Msunga ametangaz...
https://samchardtz.blogspot.com/2015/07/msaidizi-wa-naibu-katibu-mkuu-ccm-bara.html
Bw. Jumanne Juma Msunga.
Na Hillary Shoo, SINGIDA
MSAIDIZI
wa Naibu Katibu Mkuu wa (CCM) Bara, Jumanne Juma Msunga ametangaza
rasmi kuhama CCM na kujiunga na CHADEMA, kwa madai kuwa CCM ni chama
cha kudhulumu haki za wanachama wake.
Akitangaza
uamuzi wake huo jana mbele ya waandishi wa habari kwenye ofisi za
CHADEMA Mkoani Singida, Msunga alisema ameamua kujinga na CHADEMA,huku
akidai kuwa CCM haikutenda haki katika mchakato mzima wa kumpata Mgombea
wa nafasi ya Urais.
Alisema
CCM haina shukrani kwani imejaa dhuluma kwani katika mchakato huo
baadhi ya Wagombea walikatwa bila kujieleza mbele ya kamati husika.
“Kuna
viongozi wakuu wa nchi hii ambao mimi nawaheshimu kama vile Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda Makamu wa Rais Mohamed Bilal, Edward Lowassa
hawakunusa hata tano bora, hiyo sio haki ni dhuluma tu ilifanyika kwa
maslahi ya mtu mmoja, kwa hiyo mimi kama kijana nimeona nifanye maamuzi
magumu ya kuondoka ndani ya CCM.” Alisistiza Msunga.
Hata
hivyo alisema haina maana kuendele kuwa amwajiriwa wa chama ambacho
hakitendi haki na hivyo anaamini kwa kijunga kwake CHADEMA kumempatia
faraja kwani anajisikia kuwa huru sasa.
“Vijana
wenzangu huu ni wakati wa fungukeni sasa jiungeni na CHADEMA ni chama
cha nguvu ya umma na mara zote haki itatendeka huku kwani nimekuwa
kiongozi ndani ya CCM toka mwaka 2012 na ni mtumishi hadi leo hii na
hata ofisi yao bado sijaikabidhi”, alisema.