TAMKO LA MAASKOFU NA WACHUNGAJI KUTOKA MADHEHEBU MBALIMBALI JUU YA TUKIO LA KUUGUA GHAFLA ASKOFU GWAJIMA.
Sisi maaskofu na wachungaji kutoka makanisa mbalimbali tumeshtushwa na kusikitishwa kwa taarifa ya ugonjwa wa Askof...
https://samchardtz.blogspot.com/2015/03/tamko-la-maaskofu-na-wachungaji-kutoka.html
Sisi maaskofu na wachungaji kutoka makanisa mbalimbali tumeshtushwa na
kusikitishwa kwa taarifa ya ugonjwa wa Askofu na mtumishi mwenzetu
Josephat Gwajima ambaye tarehe 27/03/2015 alifika kituo cha polisi cha
kati kuitikia wito wa polisi uliomtaka kwenda kujibu shutuma za kutumia
lugha ya matusi kwa kardinali Pengo.
Tumepata fursa ya kutafakari na kujadili kwa kina hali iliyompata Askofu
mwenzetu hasa baada ya kuzingatia kuea Askofu Gwajima alifika polisi
akiwa mzima na mwenye afya njema lakini wakati wa akihojiwa na polisi,
hali yake ilibadilika ghafla kiasi cha kupelekea yeye kulazwa hospitali
ya TMJ akiugua tena kwenye wodi ya wagonjwa mahututi yaani (ICU) katika
chumba cha uangalizi maalum.
Maswali yetu makuu ni kitu gani kimempata mwenzetu? Tunajiuliza, je vyombo vya usalama vimekua sio sehemu salama kama zamani?
Tukiwa bado tunatafakari hill, tumeshtushwa tena baada ya kupata taarifa
ya kuwa Wachungaji Wasaidizi wa Askofu Gwajima pamoja na walinzi wake
waliokuwepo hospitalini hapo kwa ajili ya kumuuguza nao pia wamekamatwa
kwa tuhuma za. kutaka kumtorosha Askofu Gwajima.
Jambo hili linashangaza zaidi maana wachungaji wale wale waliokuwa naye
akiwa mzima wa afya wakati anaelekea polisi ndio wale wale wanatuhumiwa
kutaka kumtorosha akiwa mgonjwa.
Ni jambo la kushangaza na lisiloingia akilini kuwa wasaidizi hao wa
Gwajima walitaka kumtorosha wakati Gwajima kama angekua na nia hiyo
angekwisha fanya hivyo mana alikuwa na uwezo wa kutoroka alipokua Arusha
kwenye kikao cha Maaskofu wakuu wa makanisa ya Kipentekoste ambao
alipata taarifa za kuitwa Polisi.
Isitoshe Gwajima aliitija wito na kwenda polisi mwenyewe kwa miguu yake bila kushurutishwa, wala hakufikishwa polisi kwa nguvu.
Swali: Kama alikua anaona ugumu wa kutoroka wakati hakuna polisi
anayemlinda na huku akiwa mwenye afya tele, itakuaje rahisi kutoroshwa
leo akiwa mahututi na akiwa kwenye ulinzi mkali wa polisi?
Mbona hii inastaajabisha?
Mbona hii inastaajabisha?
Jambo jingine linalotupa shida ni kuhusu mlalamikaji wa kesi hii
inayomkabili Askofu Gwajima. Tumeelezwa na wasaidizi wa Askofu Gwajima
kuwa pale polisi walielezwa kuwa aliyefungua kesi hii sio Pengo ila mtu
mmoja aitwaye Aboubakar.
Kwa ufahamu wetu juu ya sheria unatutuma kuamini kuwa Aboubakar sio MTU
sahihi wa kufungua kesi hiyo sababu hawezi kutuonyesha ameumizwa kiasi
gani na matamshi ya Askofu Gwajima.
Isitoshe, Kardinali Pengo mwenyewe ametamka katika Ibada yake ya
Jumapili hii ya tarehe 29/03/2015 kuwa amemsamehe Gwajima, yupi tena
mwenye uchungu wa kumzidi Kardinali Pengo?
RAI YETU:
Rai yetu ni kwamba, ni vizuri serikali pamoja na vyombo vyake vya usalama vikatumia weledi katika kushughulikia mambo ya kidini na viongozi wake kwani yanaweza kusababisha chuki dhidi ya serikali na pia kupelekea mpasuko mkubwa wa kidini katika jamii yetu iliyo na historia nzuri ya umoja na mshikamano na ushirikiano katika matukio yote ya kimaisha.
Rai yetu ni kwamba, ni vizuri serikali pamoja na vyombo vyake vya usalama vikatumia weledi katika kushughulikia mambo ya kidini na viongozi wake kwani yanaweza kusababisha chuki dhidi ya serikali na pia kupelekea mpasuko mkubwa wa kidini katika jamii yetu iliyo na historia nzuri ya umoja na mshikamano na ushirikiano katika matukio yote ya kimaisha.
Tunaomba serikali isaidie kuondoa mkanganyiko huu na busara kubwa itumike ili kuepusha uvunjifu wa Amani katika jamii.
MAAMUZI YETU:
Jambo hili linazungumzika, maana hata hivyo tumeshaazimia kukutana na IGP ili kupata suluhisho juu ya jambo hili.
Jambo hili linazungumzika, maana hata hivyo tumeshaazimia kukutana na IGP ili kupata suluhisho juu ya jambo hili.
Kwa niaba ya maaskofu na wachungaji:
Mwenyekiti: Askofu Dr. Mgullu Kilimba
Katibu: Askofu Dr. Dramas Mukassa
Katibu: Askofu Dr. Dramas Mukassa
Na mwandishi
F.A.K
30/03/2015
F.A.K
30/03/2015