HABARI KUBWA-ASKOFU GWAJIMA AMESHINDIKANA,ATOKA HOSPITALI ASEMA HAYA,SOMA HAPA KUJUA
NA KAROLI VINSENT KILE kinachooneka Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima (pichani) ni sawa na sikio la ...
https://samchardtz.blogspot.com/2015/03/habari-kubwa-askofu-gwajima.html
NA KAROLI
VINSENT
KILE kinachooneka Askofu wa Kanisa la
Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima (pichani) ni sawa na sikio la kufa ambalo alisikii
dawa,baada ya leo kuibuka na kusema haogopi kulitetea Tamko lilotolewa na
jukwaa la kikristo nchini ambalo linawahamasisha waamini wa dini hiyo-
Kuipigia kura ya Hapana
Katiba iliyopendekezwa na Bunge Maalum la katiba,ambapo amesema atalipinga hata
kama serikali ikimwekea vikwazo.
Kauli kiongozi wa huyo
wa Kiroho ameitoa mda huu kwenye Makao Makuu ya Jeshi la polisi Mkoa wa
Kipolisi Kinondoni ambapo alipojisalimisha ili kuhojiwa mara mwisho baada ya kutoka kwenye Hospitali ya TMJ, Mikocheni Dar es Salaam alupolazwa kutokana kuugua gafla wakati akiwa kwenye mahojiano na Jeshi la polisi wiki iliyopita.
Akiongea na waandishi wa
Habari kwa kujihami mara baada ya kuhojiwa na Jeshi la Polisi Wilaya kinondoni
na kupewa Dhamana na kituoni hapo huku wakijazana waamani wake waliojitokeza na
kumpokea Askofu wao.ambapo amesema hawezi kutishika wala kuyumbika kutokana na
vikwazo anavyowekewa na Serikali juu ya kuwatetea anaodai wakristo nchini ambao
wamewekewa Katiba anayoiita ni mbovu.
“Mimi nimetoka kwa amani nashukuru sana mungu animeponya salama,ila
nasema sitoacha kusema ukweli juu ya wakristo wenzangu ambao anakandamizwa na
mifumo ya Katiba ambayo inaonekana wazi”Amesema Askofu Gwajima.
Askofu Gwajima ameongeza
kuwa kwa kuwataka viongozi wenzake kuheshimu tamko la Jukwaa la Kikristo na
hata yeye mwenyewe amesema ataliheshimu
sana.
“Nawaamomba viongozi wa dini wenzangu
tuliheshimu Tamko hili la kikristo,na endapo tukiwa tofauti tutakuwa tunakwenda
tofauti na tunajivunjia heshima kwa jamii ambapo tulionekana kuwa na msimamo
mmoja wakati tukilitoa na mimi mwenyewe nawahakikishia nitalitetea mpaka mwisho”ameongeza
Gwajima.
Alipoulizwa na
waandishi wa Habari kuhusu Afya yake amesema hawezi kuzungumzia Afya yake
akasema mwenye ruhusa ya kumsemea afya yake, akawataka waandishi kutoendelea
kumuuliza huku akiwataka waamini wake kushangilia kwa ushindi waliupata anadai
umetokana na nguvu ya mungu.
Kabla ya kulazwa katika
Hospitali ya TMJ, Askofu Gwajima alipelekwa katika Hospitali ya Polisi Kurasini
na baadaye Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambapo yeye na wafuasi wake
waligoma na kutaka atibiwe TMJ ambapo kuna daktari wake maalumu.
Baada ya kujisalimisha kwa mara ya kwanza polisi Machi 27, mwaka huu, Askofu Gwajima anadaiwa kuhojiwa kwa staili ya Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI).
Inaelezwa alihojiwa na makachero tofauti waliokuwa wakipishana katika chumba cha mahojiano na ambao wanaonekana kubobea katika taaluma hiyo.
Wakati akidhani mahojiano yamemalizika, inadaiwa waliingia maofisa wengine kumhoji maswali tofauti tofauti, mtindo ambao unatumiwa zaidi na wapelelezi wa FBI.
Hatua hiyo, pia inadaiwa kuchangia kuzimia kwake ambapo awali alidhani mahojiano yangekuwa ni kuhusu kumkashifu Kardinali Pengo tu.