Watano Wajeruhiwa Vibaya baada ya Kuangukiwa na Kifusi Cha Ukuta wa Jengo la Ghorofa 7 Jijini Mwanza
https://samchardtz.blogspot.com/2015/03/watano-wajeruhiwa-vibaya-baada-ya.html
Watu watano katika Wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza wamenusurika kifo baada ya kuangukiwa na kifusi wakati wakiwa kwenye maandalizi ya kujenga jengo lililotegemewa kuwa na ghorofa saba, eneo la Nyerere Road, jana majira ya saa sita mchana.
Akizungumza na waandishi wa habari eneo la tukio, Mkuu wa Wilaya ya
Nyamagana, Baraka Kunisaga alisema kuwa amesikitishwa na tukio hilo
ambapo watu hao wameangukiwa na ukuta wakati wakijenga msingi wa jengo
hilo na hii ni kutokana na kuwa na wakandarasi ambao hawajengi majengo
kwa kiwango kinachotakiwa.
Katika hatua nyingine, Kunisaga amesema kuwa hali ya Watanzania kuwa
wanapoteza uhai wao kila kukicha kutokana na kuangukiwa na vifusi,
serikali haiwezi kukubaliana nayo hivyo amesitisha ujenzi wa jengo hilo.
Majeruhi waliokumbwa na tukio hilo wameongea na waandishi wa habari
japo kwa taabu na kusema kuwa ukuta uliowaangukia ulikuwa umeunganishwa
kama uzio hivyo wakati wakiendelea kuchimba msingi, uzio huo ulikuwa
ukiendelea kutitia hivyo kusababisha kuporomoka na kuwaangukia.
Daktari wa zamu wodi ya dharura, Ernest Elisenguo amethibitisha
kupokea majeruhi watano ambao wametokana na tukio la kuporomokewa na
kifusi na kuwataja kuwa ni Ramadhan Hussein Nyarandu, Rashid Mkumba
Hamis, Elias Bahati, Benson Agustino na Mtani ambapo watatu kati ya hao
hali yao imeendelea vizuri na wameruhusiwa kwenda nyumbani ila wawili
kati yao bado hali zao siyo nzuri na wataendelea kuwa chini ya uangalizi
wa madaktari.
Majeruhi Rashid Mkumba Hamis, ameeleza kama ifuatavyo: "Mimi ni fundi
na nilikuwa natengeneza 'bezi' kwa ajili ya kushikilia nguzo za
ghorofa wakati ninaendelea na kazi yangu nikaanza kusikia udongo
ukiniangukia mgongoni, ghafla nikasikia matofali yananiangukia.