Flatnews

Promosheni ya Jaymillions yaanza kwa kishindo jijini dar

Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Maongezi wa Vodacom Tanzania, Samson Mongella (kushoto) akimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mtendaji wa ...


Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Maongezi wa Vodacom Tanzania, Samson Mongella (kushoto) akimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mtendaji wa AIM Group, Nadeem Juma (kulia) wakati wa hafla ya uzinduzi wa promosheni ya JayMillions iliyozinduliwa na Vodacom jijini jana. Ili kujua kama ameshinda, mteja anatakiwa kutuma neno “Jay” kwenda 15544 mara moja tu kwa siku.
Wageni waalikwa waliofika katika kuzinduzi wa promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom wakimsikiliza Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania, Abigail Ambweni (wa kwanza kushoto) akieleza jambo wakati wa hafla hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Ili kujua kama ameshinda, mteja anatakiwa kutuma neno “Jay” kwenda 15544 mara moja tu kwa siku.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa Vodacom, Rosalynn Mworia (katikati) akiteta jambo na wageni waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa promosheni ya JayMillions inayoedheshwa na kampuni hiyo iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam. Ili kujua kama ameshinda, mteja anatakiwa kutuma neno “Jay” kwenda 15544 mara moja tu kwa siku.
Meneja Masoko wa Uhuru Media, Janerose Chale (wa pili kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom, Kelvin Twissa (wa kwanza kushoto) wakati wa hafla ya uzinduzi wa promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na kampuni hiyo iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam. Ili kujua kama ameshinda, mteja anatakiwa kutuma neno “Jay” kwenda 15544 mara moja tu kwa siku.
Mtangazaji wa kituo chatelevisheni ya Taifa (TBC), Bavon Benjamin (wa kwanza kulia) akimsikiliza balozi wa promosheni ya JayMillions Hillary Daud “Zembwela” (wa tatu kulia) wakati wa hafla ya uzinduzi wa promosheni hiyo inayoendeshwa na kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Ili kujua kama ameshinda, mteja anatakiwa kutuma neno “Jay” kwenda 15544 mara moja tu kwa siku.
Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom, Kelvin Twissa (kulia) akitoa maelezo juu ya promosheni ya JayMillions iliyozinduliwa na kampuni hiyo jana wakati wa hafla ya uzinduzi iliyofanyika jana. Pamoja naye ni balozi wa promosheni hiyo, Hillary Daud “Zembwela” (kushoto). Ili kujua kama ameshinda, mteja anatakiwa kutuma neno “Jay” kwenda 15544 mara moja tu kwa siku.

Promosheni ya Jaymillions ambayo imezinduliwa na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom leo  imeanza kwa kishindo na kuleta msisimko wa wateja na wageni waalikwa waliohudhuria hafla ya uzinduzi iliyofanyika katika hoteli ya Double Tree jijini jana.

Balozi wa promosheni hiyo Hilary Daudi”JayMillions” alikuwa kivutio katika hafla hiyo alipokuwa anawauliza maswali  wageni waliohudhuria  na kuwapatia fedha taslimu waliofanikiwa kujibu maswali hayo na kutoa maelezo zaidi ni jinsi gani ya kushiriki.

Akizungumza na wageni waalikwa kwenye hafla ya uzinduzi     Mkuu  wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa ,alisema promosheni hii inayojulikana kama Jaymillions  inawahusisha wateja wote wa Vodacom “Kiasi kikubwa cha fedha kitatolewa kila siku na ni rahisi kabisa kila mtu kushiriki”Alisema

Vodacom  itatoa mshindi mmoja wa Sh.100m/- kila siku, washindi kumi wa Sh.10m/- kila siku na washindi miamoja wa Sh.1m/- KILA SIKU kwa siku mia moja! Pia washindi elfu kumi watapokea muda wa maongezi wa bure wenye thamani ya Sh. 1000/-

Twissa ameongeza kuwa inadhihirisha dhamira ya  kampuni ambayo mbali na kutoa huduma bora kwa wateja wake pia ina dhamira ya kubadilisha maisha ya wateja kuwa murua zaidi ambao wamekuwa wakiendelea kujiunga na familia ya Vodacom kila siku.

 Alisisitiza kuwa ili kushiriki katika promosheni hii, mteja yeyote wa Vodacom, aliyeko popote nchini anahitaji kutuma SMS moja tu yenye neno “JAY” kwenda namba 15544 kila siku ili kujua kama ameshinda au la. Mara tu ujumbe huu unapotumwa, mteja atapokea ujumbe mfupi utakaomjulisha kama ameshinda na ikiwa hajashinda siku hiyo atajulishwa hivyo na kuambiwa ajaribu tena siku inayofuata. Kila SMS itagharimu Sh. 300/- tu.

“”Tofauti na promosheni zilizopita, JayMillions ni rahisi sana kushiriki . Tuma ujumbe mfupi mmoja tu na mara moja tu kila siku. Hakuna maswali mengi, wala chemsha na hivyo kufanya hii kuwa promosheni inayotoa nafasi  kwa wateja wengi kuibuka washindi. Cha muhimu ni kuhakikisha kila siku unatuma ujumbe mfupi,” alieleza Twissa.


Alisema kila siku namba zilizoshinda zitapatikana kupitia mfumo mahsusi wa promosheni hii. Ili kujua kama namba ya mteja imechaguliwa, tunapenda kukusisitizia mteja wetu kutuma ujumbe mfupi wa “JAY” kila siku kwenda 15544 ili wasipoteze bahati zao iwapo namba zao zitakuwa zimechaguliwa. Bila kufanya hivyo, wanaweza kupoteza mamilioni kwani hawatoweza kujua kama namba zao zilichaguliwa kama washindi ambapo zinachaguliwa kila siku,” alisisitiza Twissa.

Post a Comment

emo-but-icon

item