Bony:Swansea yakosoa I.Coast kwa tangazo
Wilfried Bony bado hajakamilisha mpango wa kuhamia Man City ...
https://samchardtz.blogspot.com/2015/01/bonyswansea-yakosoa-icoast-kwa-tangazo.html
Klabu ya Swansea City imekosoa shirikisho la soka nchini Ivory Coast kwa kutangaza kwamba Wilfried Bony amekamilisha mpango wa kuhamia Manchester City.
Mchezaji huyo yuko nyumbani I.Coast kujiandaa kwa michuano ya mataifa ya Afrika.
Lakini msemaji wa Swansea alisema: ''kuwa klabu hio, bado haijathibitisha chochote ikiwa Bony atahama au la na kwamba Ivory Coast haina haki yoyote kutamka lolote kuhusiana na swala hilo.''
Klabu hio imeongeza kuwa Bony bado hajakamilisha mpango wake wa kuhama, na wakati atakapofanya hivyo, hilo litathibitishwa kupitia njia rasmi wala sio kupitia kwa shirikisho la soka la Ivory Coast.
Inaarifiwa klabu ya Manchester City imeshangazwa na taarifa iliyotolewa na Ivory Coast kwani inaarifiwa Bony bado hajautia saini mkataba na klabu hio.
Vilabu hivyo vilikubaliana juu ya pauni milioni 28 ili Bony kuhamia Manchester City na baada ya kuhamia klabu hiyo Man City italipa pauni nyingine milioni 3 ikiwa mchezaji huyo ataonekana kucheza vyema.
Bony alijiunga na Swansea kwa kima cha pauni milioni 12 kutoka Vitesse Arnhem mwaka 2013 na alikua mchezaji mwenye kuingiza mabao mwengi katika ligi ya Uingereza 2014 akiwa na mabao 20.