Flatnews

Picha zaonyesha uharibifu Nigeria

Picha za satelite zinazoonyesha uharibifu katika miiji ya Baga na Do...





Picha za satelite zinazoonyesha uharibifu katika miiji ya Baga na Doron Baga Kaskazini ya Nigeria

Picha za Satelite za miji ya Nigeria ambayo imesahambuliwa na Boko Haram, zinaonyesha uharibifu mkubwa uliofanyika na kuzua hofu kwamba idadi kubwa ya watu wameuawa na wapiganaji hao.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa shirika la Amnesty International.
Picha hizo zinaonyesha zaidi ya nyumba 3,700 zikiwa zimeharibiwa katika miji ya Baga na Doron Baga mwezi huu pekee.
Serikali ya Nigeria imekanusha madai kuwa takriban watu 2,000 waliuawa huku ikisema ni watu 150 pekee waliopoteza maisha.
Shirika la Amnesty limewanukuu mashahidi wakisema wapiganaji hao wa kiisilamu waliwaua watu hiholela na kuongeza kusema kuwa uharibifu uliofanyika ni wa kiwango cha kutisha.
Kumekuwa na ongezeko kubwa la mauaji yanayofanywa na Boko Haram. Katika wiki moja iliyopita, mashambulizi kadhaa yamefanyika yakiwemo yaliyofanywa na washambuliaji wa kujitoa mhanga.
Nigeria inatarajiwa kuandaa uchaguzi mkuu mwezi ujao, huku kukiwa na wasiwasi ikiwa uchaguzi wenyewe utafanyika kwa salama.
'Mji umesalia mahame'



Jeshi la Nigeria limeonekana kushindwa nguvu katika kubaliana na Boko Haram

Shirika la Amnesty lilisema katika miji ya Baga na Doron Baga, iliyo kaskazini mashariki mwa nchi, ndiko kulifanyika mashambulizi mabaya zaidi. Karibu nyumba 620 iliharibiwa mjini Baga na nyengine 3,100 kuharibiwa katika mji jirani wa Doro Baga.
Picha hizo za satelite za kabla na baada ya mashambulizi zilipigwa tarehe 2 na 7 mwezi Januari.
"Picha hizi zinaonyesha uharifi mbaya sana katika miji miwili, mmoja ambao nusura wartu wote waangamizwe katika kipindi cha siku nne pekee, '' alisema Daniel Eyre, mtafiti wa Amnesty.
''Inaonekana mashambulizi haya dhidi ya raia yalifanywa kusudi kuwaondoa katika nyumba zao huku hospitali na shule zikiteketezwa,'' alisema Daniel.
Hata hivyo mwandishi wa BBC anasema wakati picha hizo zikionyesha uharibifu uliofanyika, hazisaidii kusema idadi ya watu waliouawa.
Wiki jana afisa mmoja mkuu wa serikali, alisema kwamba wakazi wanaokimbilia maisha yao walisema mji wao abao ulikuwa na watu 10,000 kwa sasa umebaki mahame.
'Umeteketezwa karibu wote.'

Post a Comment

emo-but-icon

item