Senegal yapiga marufuku Charlie Hebdo
Jarida la Charlie Hebdo amblo limewakera waisilamu kote duniani ...
https://samchardtz.blogspot.com/2015/01/senegal-yapiga-marufuku-charlie-hebdo.html
Gazeti moja nchini Kenya, la The Star limeomba radhi kwa kuchapisha ukurasa wa kwanza wa jarida la Charlie Hebdo uliokuwa na kibonzo kinachomkejeli mtume Muhammad.
Kwingineko, Senegal imepiga marufuku usambazaji wa jarida hilo kote nchini humo.
Nchi hio pia ina uhusiano wa karibu na Ufaransa ambayo ilikuwa mkoloni wake na majarida mengi ya kifaransa yanapatikana nchini humo.
Jarida hilo limesambazwa kote duniani likuwa na kibonzo kinachomkejeli mtume akionekana kulia huku akishika bango linalosema ''Mimi ni Charlie'' huku kichwa kinachofuata kikisoma, '' Yote yamesamehewa''.
"ni hatia kwa yeyote kusambaza au kuchapisha kibonzo kilicho kwenye jarida la Charlie Hebdo kote nchini,''ilisema taarifa ya shirika la habari la APS likinukuu taarifa kutoka kwa wizara ya mambo ya ndani.
Mwandishi wa BBC nchini humo, Mamadou Moussa Ba anasema hakuna cha kushangaza kuhusiana na marufuku hio.
Raia wengi wa Senegal wamemkosoa rais Macky Sall kwa kuhudhuria maandamano nchini Ufaransa kuonyesha umoja kufuatia mauaji ya wachora vibonzo wa Charlie Hebdo na vijana waisimalu waliosema kwamba walikuwa wanalipiza kisasi kibonzo kilichochorwa awali na jarida hilo pia kumkejeli mtume.