FRANSISCO TOTTI ‘ THE KING OF ROME’, NI MKALI HADI SASA….
Labda litakuwa jambo jema sana kwa mashabiki wa klabu ya AS Roma na Italia kumuona ‘ El Capitano’ Francesco Totti akiongeza walau msimu ...
https://samchardtz.blogspot.com/2015/01/fransisco-totti-king-of-rome-ni-mkali.html
Labda litakuwa jambo jema sana kwa mashabiki wa klabu ya AS Roma na Italia kumuona ‘ El Capitano’ Francesco Totti akiongeza walau msimu mmoja ili kujaribu kuvunja rekodi iliyodumu kwa miaka 51 sasa katika kandanda la Italia. Nahodha huyo wa Roma alifunga mara mbili na kuisaidia timu yake kupata alama moja katika mchezo wa mahasimu wa Rome siku ya Jumapili.
Bao lake la kwanza alifunga kwa mguu wa kulia akiwa ndani ya eneo la hatari akimalizia pasi ya kiungo, Mholanzi, Kelvin Strochman. Lazio walikuwa mbele kwa mabao mawili kufikia nusu ya mchezo katika uwanja wa Olympic, Rome, lakini bao la Totti ambalo alifunga mara baada ya kuanza kwa kipindi cha pili liliwarudisha mchezo vijana wa kocha, Rudi Garcia na ‘ King of Rome’ akafunga bao la kusawazisha katika dakika ya 63 huku likiwa goli lake la 239 katika michezo 574.
Inashangaza kiasi kumuona Totti, 38 akiendelea kufanya vizuri kwani ni mchezaji ambaye alionekana kuandamwa na maumivu wakati mwingi wa uchezaji wake lakini ameendelea kuyashinda maumivu kwa namna ya kuvutia. Wakati mfungaji bora zaidi wa Italia, Silvio Piola alitumia michezo 619 kufunga mabao 290 katika Serie A akiwa na klabu za Pro Vercelli, Torino, Juventus na Novara kati ya miaka ya 1929-1954, Totti yuko klabuni Roma kwa maisha yake yote.
Huyu ni kijana halisi wa Rome – sehemu uliopo mji mtakatifu. Kwa mara ya kwanza Totti aliichezea Roma, 28 Machi, 1993 baada ya kocha Vujadin Boskov kumpatia nafasi katika mchezo wa kichapo cha mabao 2-0 ugenini kutoka kwa Brescia.Amecheza katika klabu moja tu maishani.
KIUNGO MSHAMBULIAJI, MSHAMBULIAJI WA PILI AU WA KWANZA,
TOTTI alifikia hatua ya kumchanganya aliyekuwa kocha wa I talia ‘ Azurri’, Dino Zofh ambaye aliwahi kukiri hadharani kabla ya kuanza kwa michuano ya Uefa Euro, 2000, Belgium & Holland kuwa hakufahamu nafasi gani ya kumpanga Totti kutokana na uchezaji wake. Italia ikiwa na washambuliaji wakali wenye uzoefu kama Roberto Baggio na Christian Vierri, Zofh alifikiria kumuanzisha mshambulizi mmoja tu kati ya wakali hao ( baggio & vierri) ili kumpatia nafasi kijana aliyekuwa na miaka 23, Totti.
Akiwa mmaliziaji mahiri klabuni kwake, makocha wengi waliofanya kazi na Totti katika timu ya Taifa walipendelea kumtumia mchezaji huyo kama kiungo-mchezesha timu mwenye uwezo mkubwa wa kutengeneza/kujitengenezea nafasi na kufunga mabao muhimu katika timu ya Italia. Akiwa ametoa pasi za mwisho 147 hadi sasa, Totti alishiriki katika nusu ya mabao ya Azurri katika michuano waliyoshuhudia wakipoteza siku ya mwisho mbele ya Ufaransa kwa kulazwa mabao 2-1 katika mchezo wa fainali.
Totti alitajwa kama mchezaji bora wa michuano hiyo ambayo wachezaji mahiri kama Luis Figo, Raul Gonzalenz, Rui Costa, Patrick Kluivert, Dennis Bergikamp, Zinedine Zidane, David Beckham na wengineo walishiriki.
Kumuona akiendelea kufanya mambo makubwa akiwa na miaka 38 sasa ni jambo la kupendeza sana kwa mchezaji huyo kipenzi cha Wataliano ambao wanaamini ndiye namba kumi ( 10 ) bora kuwahi kutokea ulimwenguni. Mshindi huyo wa taji la dunia, 2006 alipanga kustaafu soka mara baada ya kumalizika kwa msimu uliopita. Huku klabu ikiweka wazi kuwa jezi namba 10 haitatumika tena klabuni hapo kama heshima kwa mchezaji huyo.