MBUNGE WA CCM MH. CATHERINE MAGIGE AZINDUA DUKA LA VIPODOZI
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Catherine Magige (kushoto) akiwasili kuzindua rasmi duka la urembo la ZuRii House ...
https://samchardtz.blogspot.com/2015/01/mbunge-wa-ccm-mh-catherine-magige.html
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Catherine Magige
(kushoto) akiwasili kuzindua rasmi duka la urembo la ZuRii House of
Beauty linalomilikiwa na mwana Diaspora ambaye pia ni mwanalibeneke
Jestina George Meru (kulia) ndani ya jengo la Dar Free Market jijini Dar
es Salaam jana.
Na Mwandishi Wetu
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Catherine Magige leo
amezindua rasmi rasmi duka jipya la vipodozi na vitu mbalimbali
linalofahamika kwa jina la ZuRii lililopo katika jengo la Dar Free
Market lililopo katika barabara ya Alli Hassan Mwinyi Jijini Dar es
Salaam.
Akizindua duka hilo ambalo linamilikiwa na mwana Diaspora ambaye pia
ni mwanalibeneke Jestina George, Magige alisema kwamba amevutiwa na
namna Jestina alivyoweza kurudi na kuwekeza nyumbani hali ambayo
imeweza kuzalisha ajira kwa watanzania na kuwa mfano wa kuigwa.
“Kabla ya yote nachukua fursa hii kumpongeza Jestina kwani
ameonesha mfano wa umuhimu wa kujiajiri hasa kwa wanawake pia huu ni
mfano wa kuigwa kwa wanadiaspora , wengine warudi na kuja kuwekeza
nyumbani kwani fursa nyingi zipo hivyo waje wazitumie” alisema Magige.
Michuzi Media Group ikiongozwa Ahmad Michuzi mwanalibeneke wa Michuzijr Blog ( wa pili kulia) akiwa ameongozana na Mwanalibeneke wa Fullshwangwe Blog John Bukuku wakiwasili kwenye uzinduzi huo.
Aidha alitoa rai kwa wanawake wengine hapa nchini ambao wanauwezo wa
kuwa na mitaji ya kuanzisha biashara wajiajiri na kutoa ajira kwa
wengine pia natoa wito kwa watanzania wengine waje katika duka la ZuRii
kuja kutoa sapoti kwa Jestina, alisema Magige.
Wakati huohuo mmiliki wa duka hilo la ZuRii Jestina alisema kwamba
yeye ameona fursa za kuwekeza nyumbani hivyo ameamua kuzitumia
ipasavyo.
“Natoa wito kwa kwa wanadiaspora wenzangu ni kwamba wasiwe na tabia
za kuja likizo nyumbani nakuinjoi tu fedha zao tu bali wajitahidi kuja
kuwekeza kwani fursa zipo, kuanzisha duka hili ni ndoto yangu ya siku
nyingi hivyo haya ni matokeo ya njozi yangu namshukuru Mungu kwa
kutimiza ndoto hii”.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Mh. Catherine Magige
akikata utepe kuzindua rasmi duka la ZuRii House of Beauty
linalomilikiwa na Mwana Diaspora ambaye pia ni Blogger Jestina George
Meru (anayeshuhudia tukio hilo).
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Mh. Catherine Magige akiingia ndani ya duka hilo mara baada ya kulizindua.
Mmiliki wa duka la urembo la ZuRii House of Beauty na mwana Diaspora
ambaye pia ni mwanalibeneke Jestina George Meru akitoa maelezo ya baadhi
ya bidhaa zake za urembo ambazo ni original kutoka nchini Uingereza na
Marekani kwa Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Mh. Catherine
Magige. SOMA ZAIDI