LOW AWA KOCHA BORA WA DUNIA 2014
KOCHA wa Ujerumani, Joachim Low ametajwa kuwa kocha Bora wa Mwaka wa Dunia katika sherehe za FIFA utoaji tuzo za Mwanasoka Bora wa Du...
https://samchardtz.blogspot.com/2015/01/low-awa-kocha-bora-wa-dunia-2014.html
KOCHA
wa Ujerumani, Joachim Low ametajwa kuwa kocha Bora wa Mwaka wa Dunia
katika sherehe za FIFA utoaji tuzo za Mwanasoka Bora wa Dunia
zinazoendelea mjini Zurich, Uswisi.
Low
amewapiku makocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti na Atletico, Diego
Simeone kushinda tuzo hiyo baada ya kuiongoza Ujerumani kutwaa Kombe la
Dunia nchini Brazil kwa mara ya nne mwaka jana.
Mwalimu
huyo mwenye umri wa miaka 54 aliisaidia Ujerumani kumaliza ukame wa
miaka 18 wa kusubiri taji hilo kwa kuifungaArgentina katika Fainali, bao
pekee la Mario Gotze dakika
za nyongeza.