WAZIRI CHIKAWE KUFUTA USAJILI WA MAKANISA YENYE MIGOGORO KWA LENGO LA KUEPUSHA UVUNJIFU WA AMANI NCHINI
https://samchardtz.blogspot.com/2014/07/waziri-chikawe-kufuta-usajili-wa.html
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akizungumza na maelfu ya
Waumini wa Karismatiki Katoliki, Jimbo la Dar es Salaam katika maombi
maalumu kwa ajili ya kuliombea Taifa yaliyofanyika Kituo cha
Karismatiki, Ubungo jijini Dar es Salaam jana. Waziri Chikawe ambaye
alikuwa mgeni rasmi katika maombi hayo aliyataka Makanisa nchini
kudumisha amani na utulivu na kuendelea kuliombea Taifa na kuepuka
kuingia katika migogoro mbalimbali ambayo itasababisha taifa kuingia
katika uvunjifu amani makanisani. Aidha, Chikawe aliongeza kuwa migogoro
katika Makanisa na Madhehebu mbalimbali nchini imekuwa mingi katika
kipindi hiki ambapo migogoro hiyo inasababishwa na ubinafsi wa viongozi,
kutofuata Katiba na Ubadhirifu wa mali za Kanisa. Kutokana na migogoro
hiyo Chikawe alisema “Serikali haitavumilia vitendo vya uvunjifu wa
amani makanisani na ikibidi itafuta usajili wa madhehebu na makanisa
yenye migogoro ili kuepusha shari”. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kushoto) akiungana
na maelfu ya Waumini wa Karismatiki Katoliki, Jimbo la Dar es Salaam
katika maombi maalumu kwa ajili ya kuliombea Taifa. Mapombi hayo
yalifanyika katika Kituo cha Karismatiki, Ubungo jijini Dar es Salaam
jana. Waziri Chikawe ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maombi hayo
aliyataka Makanisa nchini kudumisha amani na utulivu na kuendelea
kuliombea Taifa na kuepuka kuingia katika migogoro mbalimbali ambayo
itasababisha taifa kuingia katika uvunjifu amani makanisani. Aidha,
Chikawe aliongeza kuwa migogoro katika Makanisa na Madhehebu mbalimbali
nchini imekuwa mingi katika kipindi hiki ambapo migogoro hiyo
inasababishwa na ubinafsi wa viongozi, kutofuata Katiba na Ubadhirifu wa
mali za Kanisa. Kutokana na migogoro hiyo Chikawe alisema “Serikali
haitavumilia vitendo vya uvunjifu wa amani makanisani na ikibidi itafuta
usajili wa madhehebu na makanisa yenye migogoro ili kuepusha shari”.
Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI