WENGI WAMUAGA ALIYEKUWA MHADHIRI MWANDAMIZI WA CHUO CHA UHASIBU DAR ES SALAAM
https://samchardtz.blogspot.com/2014/07/wengi-wamuaga-aliyekuwa-mhadhiri.html
Mchungaji
wa Kanisa la Moravian, Mchungaji Mwakalinga(kushoto) akiendesha Ibada
Maalum ya kumuombea Marehemu Sydney Damson kabla ya zoezi la kuuaga
mwili wa Marehemu kuanza nyumbani kwake Tandika Magorofani leo Julai 27,
2014 Temeke Jijini Dar es Salaam(wa kwanza kulia aliyeketi) ni Mtoto wa
kwanza wa Marehemu ambaye ni Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Magereza,
Masokola Damson
Baadhi
ya Watu waliojitokeza kuuaga mwili wa aliyekuwa Mhadhiri Mwandamizi wa
Chuo cha Uhasibu Dar es Salaam(TIA) wakimsikiliza Mchungaji wakati wa
Ibada Maalum ya kumuombea Marehemu iliyofanyika nyumbani kwake Tandika
Magorofani, Temeke Jijini Dar es Salaam.
Mke wa Marehemu Sydney Damson akisindikizwa na ndugu na jamaa kuuaga mwili wa Marehemu.
Mtoto
wa Marehemu, John Damson akiweka Shada la Maua katika kaburi Baba yake
baada ya kukamilisha taratibu za mazishi katika Makaburi ya Wireless,
Temeke Jijini Dar es Salaam.
Umati
wa ndugu na jamaa waliojitokeza katika mazishi ya aliyekuwa Mhadhiri
Mwandamizi wa Chuo cha Uhasibu Dar es Salaam(TIA) Marehemu Sydney Damson
ambaye amezikwa leo Julai 27, 2014 katika Makaburi ya Wireless, Temeke
Jijini Dar es Salaam(Picha na Lucas Mboje).
.Mwili
wa Marehemu Sydney Damson ambaye aliyekuwa Mhadhiri wa Chuo cha Uhasibu
Dar es Salaam(sasa kikijulikana Taasisi ya Uhasibu Tanzania) ukiwasili
nyumbani kwake Tandika Magorofani, Wilayani Temeke tayari kwa taratibu
za kuaga kabla ya kwenda mazikoni.