ALI KIBA AKIZUNGU MZIA KUHUSU UZINGUZI WA NGOMA ZAKE 2
https://samchardtz.blogspot.com/2014/07/ali-kiba-akizungu-mzia-kuhusu-uzinguzi.html
Mkali wa Bongo Fleva, Ally Saleh ‘Ali Kiba’
Habari ya
mjini kwa sasa ni uzinduzi wa nyimbo mbili za Ally Saleh ‘Ali Kiba’,
Mwana na Kimasomaso ambazo atazizindua kwenye Tamasha la Matumaini
Agosti 8, mwaka huu Uwanja wa Taifa jijini Dar.Kiba
ambaye ni mkongwe kunako muziki wa Bongo Fleva, amefunguka yeye siku
zote ni staa na huwa hakosei hivyo mashabiki watarajie burudani kali
siku hiyo.
Kiba ameizungumzia shoo yake katika tamasha hilo kwamba itakuwa spesho hivyo mashabiki wategemee mambo yafuatayo;
Kiba ameizungumzia shoo yake katika tamasha hilo kwamba itakuwa spesho hivyo mashabiki wategemee mambo yafuatayo;
Shoo kali
Katika
shoo zake zote huwa habahatishi. Amekuwa ni msanii wa kwanza kutoka
Bongo kwa kupiga idadi ya shoo nyingi nje ya nchi kuliko msanii yeyote
hata katika matamasha ya ndani ya Bongo amekuwa akiteka hisia nyingi za
mashabiki, kwenye Tamasha la Matumaini amesema itakuwa ni zaidi ya
burudani.
Kuchomoka kivingine
Baada ya kukaa kimya kwa muda sasa mfalme huyo mwenye sauti ya ajabu, sauti ya kumfanya kila shabiki aikumbuke inapopotea kidogo, amesema anakuja kivingine ambapo atapiga muziki wake kwa mpangilio maalum kuanzia sauti nzuri ya kuwabembeleza.

Habakishi kitu
Kiba amesema siku hiyo hatabakisha kitu, atazipiga nyimbo zote kali kuanzia zile za zamani kama Single Boy, Dushelele, Mac Muga, Run Dunia na nyingine kibao bila kusahau Mwana na Kimasomaso ambazo ndiyo habari ya mjini.

Tamasha
hilo linatarajiwa kupambwa na matukio kibao ya kusisimua kama ngumi za
wabunge, mechi za mpira wa miguu za wabunge na wasanii wa Bongo Fleva,
Bongo Movie bila kusahau burudani nzuri kutoka kwa wasanii wanaotamba
katika muziki wa Injili.
Burudani
zote hizo kwa pamoja, mashabiki watazishuhudia kwa mtonyo wa shilingi
elfu tano tu huku sehemu ya mapato yatakayopatikana ikipelekwa katika
mfuko wa elimu nchini