Uganda yamtema Emmanuel Okwi
https://samchardtz.blogspot.com/2014/07/uganda-yamtema-emmanuel-okwi.html
Msemaji wa timu ya Uganda, Katende Malibu, amethibitisha Okwi hayuko kambini kwani hatatumika.
UGANDA inacheza na Mauritania Agosti 2 kwenye
Uwanja wa Olympic, lakini imemwondoka kambini straika wa Yanga, Emmanuel
Okwi baada ya kuumia nyonga. Mechi hiyo ya Uganda ni kuwania kufuzu
fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon).
Msemaji wa timu ya Uganda, Katende Malibu, amethibitisha Okwi hayuko kambini kwani hatatumika.
Mastraika ambao wanabaki kwenye mpango wa kocha wa
Uganda, Sredejovic Milutin ‘Micho’ ni Geofrey Massa, Hamis Diego Kizza
na Brian Umony.