HII NDIO KAULI YA DUDUBAYA BIFU LA DIAMOND NA ALI KIBA
https://samchardtz.blogspot.com/2014/07/hii-ndio-kauli-ya-dudubaya-bifu-la.html
Dudubaya
anajulikana kama mmoja wa Wasanii wa siku nyingi bongoflevani ambae
pamoja na headlines zake binafsi huwa anasikika mara chache akizungumzia
au kutoa ushauri kwa ishu kadhaa za Wasanii wenzake.
Baada ya
kusikia yanayoendelea kati ya mastaa wa bongofleva Diamond na Ally Kiba
kwamba wako kwenye beef, Dudubaya Afunguka asema yafuatayo >>
‘Wasanii
wa Tanzania tuna wapambe na sio marafiki kwa sababu mpambe unaweza kuwa
umelewa yeye ndio anakoleza ugomvi lakini rafiki ni yule anaekuonya au
kukushauri’
‘Ali
Kiba alifanya ngoma na R.Kelly nikafurahia na nikapenda kinoma kupiga
salute kwa mdogo wangu anakwenda next level, Diamond kaja kufanya vizuri
na ninafurahiaSoma zaidi>>
muziki
huu unakosa nguvu kwa sababu ya roho mbaya, wivu na chuki na kutokuwa
makini na wanaotuzunguka, anakwenda kwa Diamond anasema hivi kisha
anakwenda kwa Ally Kiba anasema hivi’ – Dudubaya‘Ninachowashauri hawa
wadogo zangu watulie chini wajitambue ni Wasanii na usanii wao ni wa
kutengeneza pesa, tena watengeneze hata Tour ya Amani wazunguke nchi
nzima.. wazunguke hata Afrika Mashariki na sio hizi beef’
‘Siku
moja nilikua na Dully Sykes na Christian Bella alafu watu wakawa
wanasema Diamond ooohhh sijui kashindaje tuzo saba, nikawaambia hivi
ukiwa na akili timamu wimbo kama ‘my number one’ kila kona unayopita,
video mpaka TV za kimataifa zinapiga alafu leo unaweza video yako ya
kijingajinga unategemea kuishinda ‘my number one’ …….Diamond alistahili
kushinda hizo tuzo saba, mimi sikuona cha ajabu’
Kwenye
sentensi nyingine Dudubaya amesema ‘kuna gazeti moja liliandika eti
Diamond alihonga hela kuchukua hizo tuzo, ni vitu vya kipumbavu kabisa…
hujui kusoma lakini picha lazima uione, Ali Kiba na Diamond kila mmoja
ana mama yake, wakae chini kama binadamu wajitambue, waachane na mambo
ya watoto wa hapa mjini hawa ni wapambe tu mwisho wa siku hawana msaada’