Mwambusi: Yanga, Azam haziisumbui Mbeya City
Kocha wa Mbeya City, Juma Mwambusi Timu za Azam, Simba na Yanga zimeendelea na maandalizi yao kwa ajili msimu ujao ...
https://samchardtz.blogspot.com/2014/07/mwambusi-yanga-azam-haziisumbui-mbeya.html
Timu za Azam, Simba na Yanga zimeendelea na
maandalizi yao kwa ajili msimu ujao lakini Mwambusi alisema kila kocha
ana programu yake na anafahamu anachokifanya hivyo muda uliopo unamtosha
kuandaa timu ya kupambana na vigogo hivyo.
KOCHA wa Mbeya City, Juma Mwambusi amesema muda
wa wiki nne hadi sita unamtosha kuiandaa timu yake kwa ajili ya msimu
ujao, hivyo hakuona haja ya kuendelea na mazoezi wakati Ligi Kuu
Tanzania Bara imesogezwa mbele.
Timu za Azam, Simba na Yanga zimeendelea na
maandalizi yao kwa ajili msimu ujao lakini Mwambusi alisema kila kocha
ana programu yake na anafahamu anachokifanya hivyo muda uliopo unamtosha
kuandaa timu ya kupambana na vigogo hivyo.
Mwambusi alisema:“Timu nyingine zimekuwa na
maandalizi ya muda mrefu ila kwetu hilo si tatizo, nitaiandaa timu kwa
wiki nne hadi sita na itakuwa nzuri kwa ajili ya kupambana msimu ujao,
huo muda unatosha sana.”
Kwa upande mwingine kocha huyo alisema hana
taarifa zozote za kutaka kuondoka kwa mshambuliaji wa timu hiyo, Saady
Kipanga na ameshangaa kusikia amefanya mazungumzo na viongozi wa Simba
wakati bado ana mkataba na timu hiyo.
“Mchezaji yeyote anayetaka kuondoka aje tu
tuzungumze, kikubwa nitakaa na kuzungumza naye kabla ya yeye kuondoka
ila si kwamba nitamzuia. Mpaka sasa hakuna mchezaji aliyenifuata ama
kunitaarifu kuwa anataka kuondoka hivyo siwezi kuzungumza zaidi juu ya
hilo,” alisema Mwambusi