Mganga Atoweka na seheme za siri za mtoto
https://samchardtz.blogspot.com/2014/07/mganga-atoweka-na-seheme-za-siri-za.html
Mtoto Almasi mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi kumi akiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili
Katika
hali ya kushangaza madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili
(MNH), jijini Dar es Salaam walipigwa na butwaa baada ya mtoto Almasi
mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi kumi kufikishwa hospitalini hapo
akiwa amekatwa seheme zake za siri na mtu aliyedaiwa ni mganga wa
kienyeji na kukimbilia kusikojulikana.Akizungumza
kwa masikitiko makubwa wiki iliyopita, baba wa mtoto huyo, Ismail
Kamaga alisema tukio hilo lilitokea hivi karibuni katika Kijiji cha
Omukagando, Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera.
Alisema mganga huyo
aliyemtaja kwa jina moja la Adinali alifanya kitendo hicho kwa watoto
wawili akidai anawafanyia tohara.“Alidai anawafanyia tohara watoto
wawili, baada ya muda mwenzake alipona wa kwangu hakuna kitu na nyeti
aliondoka nayo, sina namna tena ya kumsaidia mwanangu.
Nilimpeleka
Hospitali ya Mugawa, Kagera ambako aliwekewa mpira wa kutolea haja
ndogo na madaktari wakasema hawana jinsi.“Pia nilikwenda Kituo cha
Polisi Karagwe kuomba msaada wa kumkamata mtuhumiwa lakini
imeshindikana,” alisema baba huyo.
Mzazi
huyo aliiomba serikali kumtafuta mtuhumiwa akisema tukio alilolifanya ni
sawa na kuuondoa uhai wa mtu.Kwa upande wake, muuguzi wa zamu aliyekuwa
hospitalini hapo, Kulwa Kaombwe alisema kitendo kilichofanywa na mtu
huyo si cha kuvumiliwa akaiomba serikali kuchukuwa hatua ili mtuhumiwa
afikishwe kwenye vyombo vya sheria.
“Kwa
ujumla huyu mtoto amebadilishiwa staili ya maisha na hicho ni kilema.
Kumkata uume maana yake mtoto huyo hatapata mke wala watoto katika
maisha yake,” alisema muuguzi huyo.
Kuhusu matibabu, alisema wanaendelea naye lakini tabu anayoipata Almasi ni kujisaidia kwa shida hasa haja kubwa.