Tambwe, Kiongera hapatoshi Simba
https://samchardtz.blogspot.com/2014/07/tambwe-kiongera-ametua-simba-akitokea.html
Kiongera ametua Simba akitokea KCB ya Kenya na sasa
atakuwa pacha wa Tambwe ambaye ni mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara msimu
uliopita kwenye safu ya ushambuliaji ya kikosi hicho.
MRUNDI Amissi Tambwe amemkaribisha straika mpya
wa Simba, Paul Kiongera, ili wapigie mabao huku Mkenya wa Azam FC,
Ibrahim Shikanda akikiri jamaa yupo vizuri sana.
Kiongera ametua Simba akitokea KCB ya Kenya na
sasa atakuwa pacha wa Tambwe ambaye ni mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara
msimu uliopita kwenye safu ya ushambuliaji ya kikosi hicho.
Tambwe aliliambia Mwanaspoti akisema: “Nimesikia
ujio wake na ninachosema, namkaribisha kwa mikono miwili aje tuifanyie
mambo Simba.
“Simjui lakini tutakapokutana naamini mambo
yatakuwa sawa, kikubwa tushirikiane. Pia ninamuasa ajitambue, awe
mvumilivu na ajitume, mtaji wa masikini ni nguvu zake mwenyewe.”
Kwa upande wa Shikanda ambaye ni kocha msaidizi wa
Azam FC, alisema: “Simba wamelamba dume aisee, kwani Kiongera ni
straika mzuri wa aina yake, ana uwezo wa juu kwenye kufunga na staili
yake ya uchezaji hakai na mpira akipata anatoa na yuko fasta.
“Ni mzuri anapocheza straika wa pili namba 10,
huwa anacheza kiungo mshambuliaji pia na akicheza pamoja na Tambwe,
wataisaidia sana klabu yao.”
Kiongera aliwahi pia kuichezea Gor Mahia na alitarajiwa kusaini Simba jana Jumatatu jioni.
BOFYA HAPA
BOFYA HAPA