Makamanda wa Kosovo washtakiwe - Ripoti
https://samchardtz.blogspot.com/2014/07/makamanda-wa-kosovo-washtakiwe-ripoti.html
Mwendesha mashtaka kutoka kwa
Jumuia ya Ulaya amesema baadhi ya viongozi wa zamani wa Jeshi la
ukombozi la Kosovo, Kosovo Liberation Army wanapaswa kufunguliwa
mashtaka ya makosa dhidi ya binadamu ikiwemo mauaji, kuweka kizuizini
watu kinyume cha sheria.
Clint Williamson alitumia miaka mitatu akifanya
uchunguzi kuhusiana na mauaji kufuatia machafuko yaliyotokea Kosovo
katika miaka 1990.Hadi hapo baadae kwa sasa hatawataja waliohusika mmoja mmoja kwa sababu wengi wao wameshika madaraka serikalini.
Tuhuma za kukata viungo vya binadamu na kuvisafirisha ni miongoni mwa makosa wanayotuhumiwa lakini hata hivyo makosa hayo ni kwa kiwango fulani.
Uchunguzi huo ulianzishwa kufuatia ripoti yenye utata iliyoandaliwa na baraza la Ulaya miaka minne iliyopita, iliyosema kuwa wakuu katika uongozi wa sasa nchini Kosovo akiwemo waziri mkuu Hashim Thaci, walihusika na biashara ya viungo vya miili ya binadamu kutoka kwa waserbia nchini Kosovo.
Hata hiyo wote hao wanakana kutenda makosa hayo.