Binamu wa Karzai auawa
https://samchardtz.blogspot.com/2014/07/binamu-wa-karzai-auawa.html
Binamu wa rais Hamid Karzai wa
Afghanistan, Hashmat Karzai ambaye ana ushawishi mkubwa nchini humo,
ameuwawa katika shambulizi la kujitoa mhanga kusini mwa mji wa Kandahar.
Msemaji wa gavana wa mkoa huo amesema Hashmat
alifariki baada ya mshambuliaji wa kujitoa mhanga kujilipua, huku
akimkumbatia katika kisingizio kwamba anampa Bwana Karzai salamu za
sherehe za Eid Ul Fitri.Ashraf alikuwa ni mmoja wa wagombea urais wawili katika uchaguzi uliokuwa na utata mwezi uliopita.
Wanahabari wanasema Hashmat alikuwa na ushawishi mkubwa huko Kandahar na pia alifahamika kama mfugaji wa simba.