UGONJWA WA AJABU WAMTESA KIJANA HUYU,MSAADA WAKO UNAHITAJIKA
https://samchardtz.blogspot.com/2014/07/ugonjwa-wa-ajabu-wamtesa-kijana.html
Kijana Lawrent Lawrian, akiwa na uvimbe wa ajabu kichwani mwake.
Lawrent
Lawrian, 42 (pichani), ni mkazi wa Kijiji cha Nyakisogo, Wilaya ya
Biharamlo, mkoani Kagera, amekuwa mwenye huzuni na kukosa raha kwa muda
wa miaka 35 kutokana na gonjwa la ajabu linalomtesa ambalo
limemsababishia mambo mengi ikiwa ni pamoja na kutoendelea na masomo.
Gonjwa
hilo la ajabu ni uvimbe kama nundu kichwani wenye uzito wa kilo 3,
ulimuanza akiwa darasa la kwanza.Akielezea zaidi kwa njia ya simu hivi
karibuni Lawrent alisema: “Gonjwa hili lilianza kama
kauvimbe nikiwa na umri wa miaka saba, wakati huo nilikuwa na wazazi
wote na ilipofika mwaka 1992 baba akafariki dunia. “Nikabakia na
mama tukawa tunaishi kwa kutegemea kilimo cha kawaida, nilikuwa nikienda
shule lakini ilifikia hatua nilishindwa kutokana na maumivu na
manyanyaso. “Darasa la saba nilimaliza kwa tabu sana, kwani
wanafunzi wenzangu walikuwa wakinicheka na kunitenga, licha ya
kuadhibiwa na walimu lakini hawakuacha tabia yao.“Kutokana na
hali hiyo, nilishindwa kuendelea na masomo kwani nilikuwa nikifungiwa
ndani ili kunipunguzia kero toka kwa wenzangu.
Kijana Lawrent Lawrian akiuguza uvimbe.
“Nilikaa
kwa kujificha hadi nilipojiona mkubwa nikaamua kuoa, sasa nina watoto
sita wanaonitegemea.“Kwa upande wa matibabu baada ya uvimbe kuwa mkubwa
nilipelekwa kwa padri mmoja katika Hospitali ya Wilaya ya Biharamulo
lakini hawakugundua tatizo kutokana na kutokuwa na vifaa vya kumpimia.
“Baadaye
kuna madaktari Wazungu walifika katika Hospitali ya Bukoba nikaenda,
waliponipima walisema ni uvimbe wa kawaida lakini hawakuweza kunitibu.
“Ilibidi
nikae nyumbani, maumivu yalizidi kuongezeka nikawa nashindwa kupata
usingizi, nikalazimika kwenda Hospitali ya Mgana, nilifanyiwa vipimo,
nao walisema ni uvimbe wa kawaida ambao unatakiwa ufanyiwe upasuaji na
nikaambiwa gharama yake ni shilingi milioni moja na laki sita,
nikashindwa kwa kuwa sina fedha hizo.
“Kwa
sasa uvimbe huu umekua mkubwa sana na ni mzito na umenifanya nishindwe
kwenda shambani, nimekuwa mtu wa kulala, familia yangu nayo inapata
shida. “Mtoto wangu wa kwanza kati ya sita yupo kidato cha pili na wote
wamekuwa wakimtegemea mama yao anayewatunza kwa kipato kidogo
kinachopatikana kutokana na kilimo cha jembe la mkono.
“Nawaomba
wasamaria wema wanisaidie kupata fedha za matibabu ili kuokoa maisha
yangu kwa kuwasiliana nami kwa namba 0714-533 430.”