HUKU WENGINE WAKIWA NA FURAHA YA KULA SIKUKUU YA IDDI LAKINI WAPALESTINA 6 WAUWAWA GAZA
https://samchardtz.blogspot.com/2014/07/huku-wengine-wakiwa-na-furaha-ya-kula.html
Wapelestina wapatao sita
wameuawa katika mashambulizi ya mabomu yaliyofanywa na Israel katika
eneo la Gaza katika siku inayohesabika kuwa ni ya mashambulizi makubwa
tangu Israel iishambulie Palestina takribani wiki tatu zilizopita.
Mwandishi wa BBC aliyepo Gaza anasema watu wa familia saba wameuawa katika mpaka baina ya Israel na Palestina uliozingirwa.Wanajeshi 10 wa Israel wameuawa siku ya Jumatatu wakiwemo wapiganaji watano wa Hamas walioingia Israel kupitia mahandaki ya chini kwa chini.
Maafisa wa afya katika utawala wa palestina wanasema kuwa watu 60 wameuawa. Israeli inasema imeshambuliwa maeneo sitini yakiwemo makao yasiyo na mtu ya kiongozi wa kundi la Hamas Ismael Haniya na vituo vya radio na runinga vya kundi la Hamas.
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema kuwa nchi yake ni lazima ijiandae kwa operesheni ya muda mrefu katika ukanda wa Gaza .
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amesema kuwa amesikitishwa na ripoti kuwa Israel ilisambaza ujumbe wa kuwaonya na kuwataka wenyeji kuondoka maeneo ya kaskazini mwa Gaza .
Ban amesema kuwa umoja wa mataifa hauna uwezo wa kuwakidhi watu zaidi wanaohama.