Bilal awaongoza maelfu ya Waumini wa Kiislam katika Swala ya Eid El Fitr katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar leo
https://samchardtz.blogspot.com/2014/07/bilal-awaongoza-maelfu-ya-waumini-wa.html
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohamed Gharib Bilal
(katikati),Sheikh Mkuu,Issa Shaaban Simba,Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam,Mh. Said Meck Sadick na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam,Sheikh Mussa Salum wakijumuika na Waumini wengine wa Dini ya
Kiislam kwenye Swala ya Eid El Fitr iliyofanyika Kitaifa kwenye Viwanja
vya Mnazi Mmoja,Jijini Dar es Salaam leo.CHANZO MTAA KWA MTAA BLOG
Sehemu ya Waumini wa Dini ya Kiislam wakiwa kwenye Ibada ya Eid el Fitr katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.
Sheikh
wa Mkoa wa Dar es Salaam,Sheikh Mussa Salum akitoa Khotuba katika Idada
ya Swala ya Eid El Fitr iliyofanyika Kitaifa kwenye Viwanja vya Mnazi
Mmoja,Jijini Dar es Salaam leo.
Mawaidha yakiendelea mara baada ya Swala ya Eid el Fitr.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohamed Gharib Bilal
akitoa salamu za Eid el Fitr leo mara baada ya Swala iliyofanyika
Kitaifa kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja,Jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Ulinzi,Dkt. Hussein Mwinyi (katikati) akijumuika pamoja na Waumini
wenzake wa Kiislam katika Swala ya Eid El Fitr iliyofanyika Kitaifa
kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja,Jijini Dar es Salaam leo.
Umati wa
Waumini wa Kiislam ukiwa katika Viwanja vya Mnazi Mmoja,Jijini Dar es
Salaam leo,tayari kwa kushiriki ibada ya Eid El Fitr.
Wakinamama pia walijitokeza kwa wingi wao kwenye Ibada hiyo.
Watangazi wa TBC Taifa wakiongozwa na Maalim Sued Mwinyi wakirusha matangazo live.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohamed Gharib Bilal
akipeana mkono wa Eid na baadhi ya Waumini wa Dini ya Kiislam mara baada
ya Swala ya Eid El Fitr iliyofanyika Kitaifa kwenye Viwanja vya Mnazi
Mmoja,Jijini Dar es Salaam leo.