FIFA inachunguza ubaguzi wa rangi
https://samchardtz.blogspot.com/2014/07/fifa-inachunguza-ubaguzi-wa-rangi.html
Fifa imeanzisha uchunguzi
kubaini ukweli wa madai ya mchezaji wa Manchester City kuwa alidhulumiwa
kutokana na rangi yake timu hiyo ilipokuwa Croatia.
Shirikisho hilo la soka duniani linaendeleza
uchunguzi huo kufuatia madai ya Seko Fofana, 20, kuwa alidhihakiwa
walipokuwa wakishiriki mechi ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 21.Msemaji wa FIFA ameiambia BBC kuwa wanakusudia kutafuta suluhu ya tukio lililompelekea kocha wa City Patrick Vieira kuwaondoa wachezaji wake uwanjani.
Kwa upande wake shirikisho la kandanda la Croatia limeanzisha uchunguzi wake.
Msemaji huyo alisema kuwa mwenyekiti wa jopo la kuchunguza dhulma kwa misingi ya rangi Jeffrey Webb anafuatilia kwa karibu matukio hayo.