KICHANGA CHAKUTWA HAI KATIKA TUMBO LA MAMA ALIYEUAWA
https://samchardtz.blogspot.com/2014/07/kichanga-chakutwa-hai-katika-tumbo-la.html
Madaktari
wa Ukanda wa Ghaza katika hospitali ya Shuhadaaul- Aqsa wamefanikiwa
kuokoa maisha ya mtoto mchanga ambaye mimba yake ilikuwa na umri wa
miezi nane na nusu kutoka katika tumbo la mama aliyeuawa shahidi kwa
hujuma ya ndege za kivita za utawala haramu wa Israel katika ukanda huo.
Kwa mujibu wa kanali ya televisheni ya al-Alam, mtoto huyo aliokolewa
baada ya kugundulika kuwa alikuwa angali hai ndani ya tumbo la mama
yake, licha ya kwamba mama yake mzazi alikuwa amekwishafariki dunia.
Habari zaidi zinasema kuwa ndege aina ya F 16 ya utawala haramu wa
Israel iliishambulia nyumba aliyokuwa akiishi Shaimaa na Ibrahim (wazazi
wa mtoto huyo) na kumuua shahidi Shaimaa huku Bwana Ibrahim akijeruhiwa
vibaya katika hujuma hiyo. Inaelezwa kuwa baada ya shambulizi hilo,
mama wa mtoto huyo aliangukiwa na vifusi vya nyumba iliyokuwa
imeharibiwa vibaya. Juhudi za waokoaji zilifanikisha kumuondoa mama wa
mtoto huyo ambaye wakati huo tayari alikuwa ameuawa shahidi huku mtoto
akionekana kuwa hai suala lililowafanya kuuharakisha mwili wa mzazi huyo
katika hospitali na kufanikiwa kuokoa maisha ya kichanga hicho