Flatnews

Wazazi wa binti mwenye ulemavu wa viungo na akili, Farida Abdalah (18) mkazi wa Lukobe Juu wameiomba Serikali, wasamaria wema na wadau mbalimbali kumsaidia binti yao huyo ambaye kwa sasa amelazwa katika hospitali ya rufaa na anaendelea kufanyiwa uchunguzi wa afya yake.

Binti Farida Abdalah (18) ambaye ni mlemavu wa viungo na akili akiwa amekaa kwenye kochi nyumbani kabla ya kupelekwa Ofisi za Dawati la Jinsia la Polisi. Picha na Hamida Shariff, Mwananchi  
  Wazazi wa binti mwenye ulemavu wa viungo na akili, Farida Abdalah (18) mkazi wa Lukobe Juu wameiomba Serikali, wasamaria wema na wadau mbalimbali kumsaidia binti yao huyo ambaye kwa sasa amelazwa katika hospitali ya rufaa na anaendelea kufanyiwa uchunguzi wa afya yake.

Pia wazazi hao ambao walionekana kuwa na hali ngumu ya kimaisha waliomba msaada wa kupatiwa matibabu ya viungo na akili kwa binti yao ili aweze kutembea na kujitambua, kwani kwa sasa binti huyo amekuwa akilala tu kitandani.

Maisha ya binti huyo ambaye umri wake haulingani na umbo lake yameguswa na watu wengi, kwani amekuwa haongei, halii, hasikii na wala hajitambui hivyo amekuwa akivalishwa nepi na kubebwa kama mtoto mchanga.

Post a Comment

emo-but-icon

item