Mahakama yamtimua waziri mkuu wa Libya
https://samchardtz.blogspot.com/2014/06/mahakama-yamtimua-waziri-mkuu-wa-libya.html
Mahakama ya juu nchini Libya
imesema kuwa kuchaguliwa kwa Ahmed Maiteg kama waziri mkuu mwezi
uliopita ulikiuka katiba ya taifa hilo.
Maiteeg aliyeapishwa kuwa Waziri mkuu mwezi uliopita na bunge la taifa ,baada ya kura iliyokumbwa na utata.
Makundi ya Waislamu yanatawala sehemu kubwa ya Libya
Hata hivyo taifa hilo limegawanyika kati ya waislamu wa kadri na wale wenye misingi kali ya dini.
Mirengo hiyo ya waislamu ndiyo yanayodhibiti maeneo tofauti ya Taifa hilo.
Uchaguzi unatarajiwa kufanyika terehe 25 June,kuchagua bunge la taifa litakalorithi nafasi inashikiliwa kwa sasa na kongamano la kitaifa al maarufu '' General National Congress'' .