WANANCHI WAELEZA MAFANIKIO YA UTAFITI RAGHBISHI WA TGNP
https://samchardtz.blogspot.com/2014/06/wananchi-waeleza-mafanikio-ya-utafiti.html
Baadhi
ya wanaharakati ngazi ya jamii wakielezea mafanikio ya utafiti wa
kiraghbishi unaofanywa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) katika
maeneo yao ulivyokuwa chachu ya baadhi ya mabadiliko kwenye mkutano jijini Dar es Salaam
Bi. Marjorie Mbilinyi mwanachama wa TGNP Mtandao akiwasilisha mada katika semina hiyoBaadhi
ya washiriki wa semina ya kutathimini utafiti wa kiraghbishi uliofanywa
na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) katika baadhi ya kata za mikoa ya
Morogoro, Shinyanga, Mbeya, Mara na Jijini Dar es Salaam wakifuatilia
mada.Baadhi
ya washiriki wa semina ya kutathimini utafiti wa kiragibishi uliofanywa
na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) katika baadhi ya kata za mikoa ya
Morogoro, Shinyanga, Mbeya, Mara na Jijini Dar es Salaam wakifuatilia
mada.Mmoja
wa washiriki wa semina ya kutathimini utafiti wa kiraghbishi uliofanywa
na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) katika baadhi ya kata za mikoa ya
Morogoro, Shinyanga, Mbeya, Mara na Jijini Dar es Salaam akichangia
mada. Semina hiyo ya mrejesho ilishirikisha wadau mbalimbali kutoka
serikalini na asasi binafsi.Baadhi
ya wanaharakati ngazi ya jamii wakielezea mafanikio ya utafiti wa
kiragibishi unaofanywa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) katika
maeneo yao ulivyokuwa chachu ya baadhi ya mabadiliko kwenye mkutano
jijini Dar es Salaam.
WANAHARAKATI
ngazi ya jamii kutoka mikoa ya Morogoro, Shinyanga, Mbeya, Mara na
Jijini Dar es Salaam wamesema utafiti wa kiraghbishi unaofanywa na
Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) katika maeneo yao unaleta mafanikio
kwani changamoto zinazoibuliwa katika maeneo ya utafiti baadhi zimeaza
kufanyiwa kazi.
Kuanzia
Machi 9 hadi 31, mwaka huu TGNP Mtandao iliendesha utafiti wa
kiragibishi kwa kuishirikisha jamii katika kata tano za Mondo
(Shinyanga), Tembela (Mbeya), Kiroka (Morogoro), Nyamaraga (Mara) na
Kata ya Mabibo ya jijini Dar es Salaam ambapo jamii iliibua kero katika
maeneo yao na kupaza sauti kwa mamlaka husika kuchochea mabadiliko.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam mwanaharakati ngazi ya jamii, Leah Peter kutoka
Kata ya Mondo, Wilaya ya Kishapu kwa niaba ya wenzake alisema kero
lilizoibuliwa katika utafiti baadhi zimeanza kushughulikiwa na mamlaka
husika.
Bi.
Peter alisema eneo lao wakati unaendeshwa utafiti wananchi
walilalamikia kitendo cha wajawazito wanaohudumiwa katika Zahanati ya
Mondo, wilayani Kishapu kulipishwa shilingi 500 kulipia kadi ambayo
imeandikwa 'haiuzwi' kitendo ambacho kwa sasa hakifanyiki tena baada ya
kupaza sauti.
Mmoja
wa washiriki wa semina ya kutathimini utafiti wa kiragibishi uliofanywa
na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) katika baadhi ya kata za mikoa ya
Morogoro, Shinyanga, Mbeya, Mara na Jijini Dar es Salaam akichangia
mada. Semina hiyo ya mrejesho ilishirikisha wadau mbalimbali kutoka
serikalini na asasi binafsi.
Mmoja
wa washiriki wa semina ya kutathimini utafiti wa kiragibishi uliofanywa
na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) katika baadhi ya kata za mikoa ya
Morogoro, Shinyanga, Mbeya, Mara na Jijini Dar es Salaam akichangia
mada. Semina hiyo ya mrejesho ilishirikisha wadau mbalimbali kutoka
serikalini na asasi binafsi.
"...Eneo
letu awali wajawazito katika Zahanati ya Mondo tulikuwa tukidaiwa
shilingi 500 kulipia kadi ya kliniki ambayo ina maandishi ya 'haiuzwi'
kitendo hiki kwa sasa hakifanyiki tena na kila muhudumu wa zahanati hiyo
kawa mlinzi wa mwenzake hili tunajivunia," alisema Bi. Peter.
Alisema
mabadiliko mengine ni pamoja na mikutano ya mapoto na matumizi ya
vijiji kufanyika jambao ambalo walililalamikia wananchi kuwa lilikuwa
halifanyiki, alisema huduma za maji ambazo ni kero eneo hilo kwa sasa
halmashauri imeleta shirika linaloendelea na maandalizi ya kuchimba
visima vya maji katika shule za msingi Kabila na Buganika. Alisema na
Shule ya Msingi Mwigumbi imepata madawati jambo ambalo lilikuwa kero.
Kwa
upande wake Bi. Neofita Kunambi kutoka Mtaa wa Azimio Mabibo jijini Dar
es Salaam alisema kero ya ngoza maarufu kwa jina la 'vigodoro'
zimepigwa marufuku eneo lao baada ya kulalamikiwa, huku amri ya
wajawazito wanaojifungulia katika Hospitali ya Parestina kutakiwa kwenda
na ndoo ya kubeba kondo la uzazi ikipigwa marufuku jambo ambalo
liliibuka katika utafiti ragibishi eneo hilo.
Aidha
alisema wanajamii eneo hilo pia walilalamikia kupanda kwa bei za maji
huku kila muuzaji akiuza bei atakayo kero ambayo imeanza kusikika kwani
sasa bei zimepungua tofauti na ilivyokuwa awali. "...Maji eneo letu kila
muuzaji alikuwa na bei yake lakini sasa imeshuka waliokuwa wakiuza
miambili ndoo sasa wanauza 100, hili pia lililalamikiwa na wananchi
kwenye utafiti," alisema Bi. Kunambi.
Kwa
mujibu wa taarifa ya pamoja ya mafanikio ya utafiti huo Kata ya
Nyamaraga mkoani Mara imefanikiwa kupaza sauti kupinga zoezi la
bomoabomoa iliyotaka kutekelezwa eneo hilo bila wahusika kulipwa haki
zao, huku wananchi wa Kata ya Mondo Kishapu kuandamana wakati wa ziara
ya Waziri wa Maji eneo hilo kudai maji safi na salama.
Taarifa
ilifafanua kuwa Kata ya Kiroka utafiti umesaidia watendaji wa huduma ya
afya kuwajibika na kuwasikiliza wananchi na suala la kero ya
upatikanaji wa dawa imebadilika tofauti na ilivyokuwa awali. TGNP
Mtandao imewakutanisha baadhi ya wanaharakati ngazi ya jamii kutuka
maeneo ya utafiti jijini Dar es Salaa ili kwa pamoja kutathimini matokeo
ya utafiti huo na kuwashirikisha kutoa mapendekezo na mikakati ya
kufanya kwa jamii ili kuchochea mabadiliko zaidi.