Flatnews

TANZANIA NA UGANDA KUUMANA DAR.


Winga machachari wa Tanzania Mrisho Ngassa akiminyana na beki wa Uganda.
Winga machachari wa Tanzania Mrisho Ngassa akiminyana na beki wa Uganda.
Katika kuelekea mchezo wa kimataifa wa kusaka nafasi ya kushiriki fainali za kombe la mataifa ya Afrika 2015 nchini Morocco Tanzania na Uganda zimepanga kukutana katika mchezo wa kujipima nguvu kabla timu hizo zote mbili hazija cheza michezo ya raundi ya pili ya kusaka nafasi ya kuingia hatua ya makundi kuelekea AFCON.
Taarifa kutoka ndani ya shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF zinasema kuwa tayari wamefanya mazungumzo na FUFA na tayari wamefikia muafaka wa timu hizo mbili kupimana nguvu.
Chanzo chetu kinasema kuwa mchezo huo utapigwa katika jiji la Dar es salaam hapo tarehe zitakapo pangwa.
Mchezo huo ni muhimu kwa timu zote mbili Tanzania na Uganda  ambazo zote zimefanikiwa kuingia katika hatua ya pili ya kusaka namba ya kucheza AFCON mwakani nchini Morocco.
Tanzania ilifanikiwa kuitupa nje ya michuan hiyo Zimbabwe kwa jumla ya mabao 3-2 baada ya Dar es salaam kushinda 1-0 na mchezo wa marudiano Harare timu hizo zikatoka sare ya 2-2 na Stars kufuzu kwa faida ya ushindi wa nyumbani wa bao 1-0.
Stars itakuwa na kibarua cha kuitoa Msumbiji katika hatua ya pili ili iweze kuingia katika hatua ya makundi.
Uganda wao wanacheza na Tanzania kujewaka vizuri baada ya kufanikiwa kuwatoa Madagascar na sasa itakuwa na kibarua cha kuitoa Equatorial Guinea katika hatua ya pili.

Post a Comment

emo-but-icon

item