Flatnews

BRAZIL MGOMO WAZIDI KUPAMBA MOTO.


Msongamano wa magari nchini Brazil baada ya mgomo wa madereva wa usafiri wa uma.
Msongamano wa magari nchini Brazil baada ya mgomo wa madereva wa usafiri wa uma.
Zikiwa zimebaki siku mbili michuano ya fainali za kombe la Dunia zianze kutimua vumbi nchini Brazil Wafanyikazi wa usafiri wa mjini Sao Paulo wamepiga kura kuidhinisha mgomo wao uendelee kwa mda usiojulikana licha ya uamuzi wa mahakama ya kazi nchini humo kuwaamuru waendelee kufanya kazi kama zamani.
Mahakama imesema wakuu katika vyama vya wafanyikazi hao wa usafiri wa mjini Metro, walitumia  mamlaka yao vibaya kwa kuanzisha mgomo tangu alhamisi iliyopita huku nusu ya vituo vya usafiri vikiwa tayari vimefungwa, msongamano wa magari umezidi kuizonga Sao Paulo.
Sasa wasiwasi unaongezeka, huku kilamtu akijiuliza Je hali ikiendelea hivyo itakuaje hapo alhamisi wakati jiji hilo ndilo linafungua dimba hilo?
Wafanyikazi hao wanadai nyongeza ya mshahara ya asilimia 12 ilhali serkali imesema itamudu nyongeza ya takrban asilimia 9.

Post a Comment

emo-but-icon

item