RAIS JAKAYA KIKWETE KUWASILI DODOMA JUMATANO JUNI 11
https://samchardtz.blogspot.com/2014/06/rais-jakaya-kikwete-kuwasili-dodoma.html
Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Jakaya Kikwete ambapo anatarajiwa kwenda ikulu siku ya jumatano.
Aidha, Rais ataongoza kikao cha Baraza la Mawaziri kitakachopewa muhtasari kuhusu Bajeti ya Serikali ya mwaka ujao wa fedha na baadaye atafuatilia uwasilishaji wa bajeti hiyo bungeni akiwa Dodoma.
Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salva Rweyemamu alisema asingeweza kuzungumzia suala hilo kwa kuwa yuko likizo lakini akaweka bayana kwamba kwa kawaida kabla ya bajeti kuwasilishwa bungeni, lazima Baraza la Mawaziri lipewe muhtasari wa bajeti husika.
Kwa upande mwingine mwaka jana kabla ya kusomwa kwa bajeti ya 2013/14, Rais Kikwete alikuwa Dodoma ambapo alikutana na mawaziri, pia alifanya kikao na Kamati ya Bunge ya Bajeti.