Kombe la Dunia 2014: Hawa hapa wachezaji wote 736 kutoka nchi 32 watakaokipiga nchini Brazil; Ribery, Tevez, Falcao, Reus, Negredo, Nasri jukwaani
Nchi zote 32 ambazo zitashiriki fainali za Kombe la Dunia nchini Brazil ambapo awali ziliwataja wachezaji 30 wa maangalizi na walita...
https://samchardtz.blogspot.com/2014/06/kombe-la-dunia-2014-hawa-hapa-wachezaji.html
Nchi
zote 32 ambazo zitashiriki fainali za Kombe la Dunia nchini Brazil
ambapo awali ziliwataja wachezaji 30 wa maangalizi na walitakiwa kutaja
wachezaji 23 tu hadi kufikia Juni 2 kwa ajili ya mashindano hayo makubwa
Ulimwenguni kwa upande wa kandanda, tayari nchi hizo zimeanza kuwasili
nchini Brazil zikiwa na wachezaji 23 kila moja tayari kuanza mashindano
hayo.
Jambo
kubwa na linaloshangaza na ambalo huenda likaondoa msisimko wa
mashindano hayo mwaka huu, ni kutkosekana kwa majina makubwa ambayo
yamekuwa yakifanya vizuri kwenye ligi kuu mbalimbali barani Ulaya.
Radamel Falcao, Franky Ribery, Reus hawatokuwepo kwenye timu zao kutokana na majeraha yanayowakabili.
Lakini
majina makubwa kama Carlos Tevez, Samir Nasri, Negredo, Donovan na
wengine mashuhuri hawatokuwepo kutokana na machaguo ya makocha.
Ifuatayo ni orodha ya
wachezaji wa kila nchi ambao wametajwa kuziwakilisha nchi zao katika
fainali za mwaka huu nchini Brazil. Wachezaji 736 kuziwakilisha nchi 32
ikiwa kila nchi imepeleka wachezaji 23.
Kundi A
Brazil
Brazil iliwataja wachezaji
wake 23 lakini ikiwaacha wachezaji wa AC Milan Kaka na Robinho katika
kikosi chake. Wachezaji wanne wa Chelsea David Luiz, Oscar, Ramires na
Willian wameitwa. Mlinda mlango wa QPR Julio Cesar ambaye yupo kwa mkopo
Toronto FC, pia amejumuishwa.
Kikosi kamili:
Walinda mlango: Julio Cesar (Toronto FC, kwa mkopo akitokea QPR), Jefferson (Botafogo), Victor (Atletico Mineiro).
Walinzi:
Marcelo (Real Madrid), Daniel Alves (Barcelona), Maicon (AS Roma),
Maxwell, Thiago Silva (wote Paris St-Germain), David Luiz (Chelsea),
Dante (Bayern Munich), Henrique (Napoli).
Viungo: Paulinho (Tottenham
Hotspur), Ramires , Willian, Oscar (wote Chelsea), Hernanes (Inter
Milan), Luiz Gustavo (Wolfsburg), Fernandinho (Manchester City).
Washambuliaji: Bernard
(Shakhtar Donetsk), Neymar (Barcelona), Fred (Fluminense), Jo (Atletico
Mineiro), Hulk (Zenit St Petersburg).
Wachezaji wa dharura: Diego
Cavalieri (Fluminese) Miranda, Filipe Luis (both Atletico Madrid),
Rafinha (Bayern Munich), Lucas Leiva (Liverpool), Lucas Moura (Paris
St-Germain), Alan Kardec (Sao Paulo).
Croatia
Croatia wachezaji wawili
wanaokipiga nchini English katika kikosi cha wachezaji 23. Mlinzi wa
Southampton Dejan Lovren, mshambuliaji wa Hull Nikica Jelavic na kiungo
wa QPR Niko Kranjcar walikuwemo kwenye kikosi cha maangalizi cha kocha
Niko Kovac, lakini Kranjcar aliondolewa kutokana na majeruhi. Mchezaji
muhimu wa Croatia anayekipiga Real Madrid kiungo Luka Modric, ameitwa.
Kikosi kamili:
Walinda mlango: Stipe Pletikosa (Rostov), Danijel Subasic (Monaco), Oliver Zelenika (Dinamo Zagreb).
Walinzi: Darijo Srna (Shakhtar
Donetsk), Dejan Lovren (Southampton), Vedran Corluka (Lokomotiv
Moscow), Gordon Schildenfeld, Danijel Pranjic (wote Panathinaikos),
Domagoj Vida (Dynamo Kiev), Sime Vrsaljko (Genoa).
Viungo: Luka Modric (Real
Madrid), Ivan Rakitic (Sevilla), Ognjen Vukojevic (Dynamo Kiev), Ivan
Perisic (Wolfsburg), Mateo Kovacic (Inter Milan), Marcelo Brozovic
(Dinamo Zagreb), Sammir (Getafe), Ivan Mocinic (Rijeka).
Washambuliaji: Mario Mandzukic
(Bayern Munich), Ivica Olic (Wolfsburg), Eduardo (Shakhtar Donetsk),
Nikica Jelavic (Hull City), Ante Rebic (Fiorentina).
Mexico
Mexico imewataja kikosi chake
cha wachezaji 23, huku fowadi wa Manchester United Javier Hernandez
akiwa mchezaji pekee wa Premier League kwenye kikosi hicho. Mlinzi wa
zamani wa Barcelona Rafael Marquez na fowadi wa Villarreal Giovani Dos
Santos wamejumuishwa lakini Carlos Vela anaendelea kukosekana kimataifa.
Kikosi kamili:
Walinda mlango: Jose de Jesus Corona (Cruz Azul), Guillermo Ochoa (Ajaccio), Alfredo Talavera (Toluca).
Walinzi: Miguel Layun
(America), Carlos Salcido (Tigres), Paul Aguilar (America), Andres
Guardado (Bayer Leverkusen), Hector Moreno (Espanyol), Francisco Javier
Rodriguez (America), Diego Reyes (Porto), Rafael Marquez (Leon).
Viungo: Miguel Angel Ponce
(Toluca), Jose Juan Vazquez (Leon), Luis Montes (Leon), Hector Herrera
(Porto), Isaac Brizuela (Toluca), Marco Fabian (Cruz Azul), Carlos Pena
(Leon).
Washambuliaji: Oribe Peralta
(Santos), Javier Hernandez (Manchester United), Giovani dos Santos
(Villarreal), Raul Jimenez (America), Alan Pulido (Tigres).
Cameroon
Kikosi
cha Cameroon cha wachezaji 23 hakina mshangao mkubwa kikiwa na
mshambuliaji wa Chelsea Samuel Eto'o na mfungaji wa magoli 16 wa Lorient
Vincent Aboubakar. Mohamadou Idrissou ameondolewa baada ya kukosa
penalti kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Paraguay.
Kikosi kamili:
Walinda mlango: Loic Feudjou (Coton Sport), Charles Itandje (Konyaspor), Sammy Ndjock (Fethiyespor).
Walinzi: Benoit Assou-Ekotto
(QPR, on loan from Tottenham Hotspur), Henri Bedimo (Lyon), Aurelien
Chedjou (Galatasaray), Cedric Djeugou (Coton Sport), Nicolas Nkoulou
(Marseille), Dany Nounkeu (Besiktas), Allan Nyom (Granada).
Viungo: Enoh Eyong
(Antalyaspor), Jean Makoun (Rennes), Joel Matip (Schalke), Stephane Mbia
(Sevilla, on loan from QPR), Benjamin Moukandjo (Nancy), Landry Nguemo
(Bordeaux), Edgar Salli (Lens), Alex Song (Barcelona).
Washambuliaji: Vincent
Aboubakar (Lorient), Eric-Maxim Choupo Moting (Mainz), Samuel Eto'o
(Chelsea), Fabrice Olinga (Malaga), Achille Webo (Fenerbahce).
Kundi B
Uhispania
Mabingwa
watetezi Uhispania imemtaja mshambuliaji majeruhi mzaliwa wa Brazil
Diego Costa na fowadi wa Chelsea Fernando Torres katika kikosi chake cha
wachezaji 23.
Kiungo wa Bayern Munich Thiago Alcantara atakosa mashindano ya mwaka huu baada ya kuumia goti hivyo akajiondoa.
Wachezaji wawili wa Manchester
City Alvaro Negredo na Jesus Navas ni miongoni mwa majina makubwa
yaliyokatwa kutoka kwenye kikosi cha wachezaji 30.
Kikosi kamili:
Walinda mlango: Iker Casillas (Real Madrid), Pepe Reina (Napoli), David De Gea (Manchester United).
Walinzi: Sergio Ramos (Real
Madrid), Gerard Pique (Barcelona), Raul Albiol (Napoli), Cesar
Azpilicueta (Chelsea), Juanfran (Atletico Madrid), Jordi Alba
(Barcelona).
Viungo: Xavi (Barcelona), Xabi
Alonso (Real Madrid), Sergio Busquets (Barcelona), Andres Iniesta
(Barcelona), Cesc Fabregas (Barcelona), Santi Cazorla (Arsenal), Koke
(Atletico Madrid), Javi Martinez (Bayern Munich).
Washambuliaji: David Silva
(Manchester City), Diego Costa (Atletico Madrid), Fernando Torres
(Chelsea), Pedro (Barcelona), Juan Mata (Manchester United), David Villa
(Atletico Madrid).
Uholanzi
Boss wa Uholanzi Louis van
Gaal amewataja wachezaji 23 sita kati yao wakikipiga kwenye soka la
British. Mshambuliaji Robin van Persie, ambaye atacheza chini ya meneja
huyo kwenye klabu ya Manchester United msimu ujao yumo kikosini na
mlinzi wa Aston Villa Ron Vlaar na kiungo wa Norwich Leroy Fer.
Rafael van der Vaart aliondolewa kwenye kikosi cha maangalizo kwa sababu ya kuumia.
Kikosi kamili:
Walinda mlango: Jasper Cillessen (Ajax), Tim Krul (Newcastle), Michel Vorm (Swansea)
Walinzi: Daley Blind, Joel
Veltman (both Ajax), Stefan de Vrij, Daryl Janmaat, Terence Kongolo,
Bruno Martins Indi, (wote Feyenoord), Paul Verhaegh (FC Augsburg), Ron
Vlaar (Aston Villa).
Viungo: Jordy Clasie
(Feyenoord), Jonathan de Guzman (Swansea), Nigel de Jong (AC Milan),
Leroy Fer (Norwich), Arjen Robben (Bayern Munich), Wesley Sneijder
(Galatasaray), Georginio Wijnaldum (PSV Eindhoven).
Washambuliaji: Memphis Depay
(PSV Eindhoven), Klaas-Jan Huntelaar (Schalke 04), Dirk Kuyt
(Fenerbahce), Jeremain Lens (Dynamo Kiev), Robin van Persie (Manchester
United).
Chile
Chile imewataja wachezaji 23
ambao inamjumuisha kikosini kiungo wa Juventus Arturo Vidal licha ya
mchezaji huyo, 26 kufanyiwa upasuaji karibuni kufuatia matatizo ya goti.
Mshambuliaji wa Barcelona Alexis Sanchez anaungana na Gary Medel,
Gonzalo Jara na Jean Beausejour. Mshambuliaji Esteban Paredes
amejumuishwa licha ya kuondolewa awali kwenye kikosi cha maangalizi.
Kikosi kamili:
Walinda mlango: Claudio Bravo (Real Sociedad), Johnny Herrera (Universidad de Chile), Cristopher Toselli (Universidad Catolica)
Walinzi: Gary Medel (Cardiff
City), Gonzalo Jara (Nottingham Forest), Jose Rojas (Universidad de
Chile), Eugenio Mena (Santos), Mauricio Isla (Juventus).
Viungo: Jorge Valdivia
(Palmeiras), Felipe Gutierrez (Twente), Jose Pedro Fuenzalida (Colo
Colo), Francisco Silva (Osasuna), Arturo Vidal (Juventus), Charles
Aranguiz (Internacional), Marcelo Diaz (Basel), Carlos Carmona
(Atalanta), Miiko Albornoz (Malmo).
Washambuliaji: Alexis Sanchez
(Barcelona), Esteban Paredes (Colo Colo) Eduardo Vargas (Valencia), Jean
Beausejour (Wigan Athletic), Mauricio Pinilla (Cagliari), Fabian
Orellana (Celta).
Australia
Australia imewaita kikosini
wachezaji wawili wa League One, Bailey Wright na Massimo Luongo, katika
kikosi cha maandalizi. Kiungo wa Crystal Palace Mile Jedinak na mlinzi
wa Newcastle Curtis Good, aliyeko kwa mkopo Dundee United, walikuwa ni
wachezaji wawili pekee wa Premier League lakini hakukuwa na nafasi
kwenye kikosi kwa Lucas Neill.
Kikosi kamili:
Walinda mlango: Mark
Birighitti (Newcastle Jets), Eugene Galekovic (Adelaide United),
Mitchell Langerak (Borussia Dortmund), Mat Ryan (Club Brugge).
Walinzi: Jason Davidson
(Heracles Almelo), Ivan Franjic (Brisbane Roar), Ryan McGowan (Shandong
Luneng Taishan), Matthew Spiranovic (Western Sydney Wanderers), Alex
Wilkinson (Jeonbuk Hyundai), Luke Wilkshire (Dinamo Moscow), Bailey
Wright (Preston North End).
Viungo: Oliver Bozanic
(Luzern), Mark Bresciano (Al Gharafa), James Holland (Austria Vienna),
Mile Jedinak (Crystal Palace), Massimo Luongo (Swindon Town), Matthew
McKay (Brisbane Roar), Mark Milligan (Melbourne Victory), Tommy Oar
(Utrecht), Tommy Rogic (Melbourne Victory), James Troisi (Melbourne
Victory), Dario Vidosic (Sion).
Washambuliaji: Tim Cahill (New
York Red Bulls), Ben Halloran (Fortuna Dusseldorf), Josh Kennedy
(Nagoya Grampus 8), Matthew Leckie (FSV Frankfurt 1899), Adam Taggart
(Newcastle Jets).
Kundi C
Colombia
Mshambuliaji
wa Colombia Radamel Falcao alitajwa kwenye kikosi cha wachezaji 30
licha ya kutocheza tangu Januari kufuatia kusumbuliwa majeraha. Mlinzi
aliyeko kwa mkopo West Ham Pablo Armero ni mchezaji pekee wa Premier
League kujumuishwa.
Kikosi kamili:
Walinda mlango: David Ospina (Nice), Faryd Mondragon (Deportivo Cali), Camilo Vargas (Independiente Santa Fe).
Walinzi: Mario Yepes (AC
Milan), Cristian Zapata (AC Milan), Pablo Armero (West Ham, on loan from
Napoli), Camilo Zuniga (Napoli), Aquivaldo Mosquera (Club America),
Santiago Arias (PSV Eindhoven), Luis Amaranto Perea (Cruz Azul), Eder
Alvarez Balanta (River Plate), Carlos Valdes (San Lorenzo).
Viungo: Fredy Guarin (Inter
Milan), Juan Cuadrado (Fiorentina), Victor Ibarbo (Cagliari), James
Rodriguez (Monaco), Abel Aguilar (Toulouse), Juan Fernando Quintero
(Porto), Carlos Sanchez (Elche), Macnelly Torres (Al Shabab), Aldo Leao
Ramirez (Morelia), Edwin Valencia (Fluminense), Alexander Mejia
(Atletico Nacional), Elkin Soto (Mainz).
Washambuliaji: Radamel Falcao
(Monaco), Luis Fernando Muriel (Udinese), Jackson Martinez (Porto),
Carlos Bacca (Sevilla), Adrian Ramos (Hertha Berlin), Teofilo Gutierrez
(River Plate).
Ugiriki
Mshambuliaji wa Fulham
Konstantinos Mitroglou amejumuishwa kwenye kikosi cha wachezaji 23 licha
ya kucheza kwa dakika 120 tangu aliposainishwa mwezi Januari kufuatia
kusumbuliwa na majeruhi. Mchezaji mwenza wa Cottagers Giorgos Karagounis
na mchezaji wa Celtic Georgios Samaras wameitwa pia.
Kikosi kamili:
Walinda mlango: Orestis Karnezis (Granada), Panagiotis Glykos (PAOK), Stefanos Kapino (Panathinaikos).
Walinzi: Kostas Manolas,
Giannis Maniatis, Jose Holebas (all Olympiakos), Sokratis
Papastathopoulos (Borussia Dortmund), Giorgios Tzavellas (PAOK), Loukas
Vyntra (Levante), Vasilis Torosidis (Roma), Vangelis Moras (Verona).
Viungo: Alexandros Tziolis
(Kayserispor), Andreas Samaris (Olympiakos), Kostas Katsouranis (PAOK),
Giorgos Karagounis (Fulham), Panagiotis Tachtsidis (Torino), Ioannis
Fetfatzidis (Genoa), Lazaros Christodoulopoulos (Bologna), Panagiotis
Kone (Bologna).
Washambuliaji: Dimitris
Salpingidis (PAOK), Giorgios Samaras (Celtic), Konstantinos Mitroglou
(Fulham), Theofanis Gekas (Konyaspor).
Ivory Coast
Mshambuliaji
wa Galatasaray Didier Drogba, 36, anajiandaa kucheza fainali za tatu na
fainali hizi zitakuwa za mwisho baada ya kutajwa kwenye kikosi cha
wachezaji 23. Ndugu wawili Yaya na Kolo Toure wanajiunga na wachezaji
wenza wa Premier League Cheick Tiote na Wilfried Bony.
Kikosi kamili:
Walinda mlango: Boubacar Barry (Lokeren), Sylvain Gbohouo (Sewe Sport), Sayouba Sande (Stabaek).
Walinzi: Kolo Toure
(Liverpool), Sol Bamba (Trabzonspor), Didier Zokora (Trabzonspor), Serge
Aurier (Toulouse), Arthur Boka (Stuttgart), Ousmane Viera Diarrassouba
(Caykur Rizespor), Constant Djakpa (Frankfurt), Jean-Daniel Akpa-Akpro
(Toulouse).
Viungo: Yaya Toure (Manchester
City), Cheik Tiote (Newcastle), Serey Die (Basel), Max Gradel (Saint
Etienne), Diomande Ismael (Saint Etienne), Didier Ya Konan (Hannover),
Mathis Bolly (Dusseldorf).
Washambuliaji: Gervinho
(Roma), Didier Drogba (Galatasaray), Salomon Kalou (Lille), Wilfried
Bony (Swansea), Giovanni Sio (Basel).
Japan
Japan imewaita kikosini
wachezaji 12 wanaokipiga Ulaya katika kikosi chake cha wachezaji 23,
akiwemo kiungo wa Manchester United Shinji Kagawa na mlinzi wa
Southampton Maya Yoshida. Kiungo wa AC Milan Keisuke Honda pia ameitwa
sanjari na kiungo wa Gamba Osaka Yasuhito Endo aliyeichezea Japan mechi
141.
Kikosi kamili:
Walinda mlango: Eiji Kawashima (Standard Liege), Shusaku Nishikawa (Urawa Reds), Shuichi Gonda (FC Tokyo).
Walinzi: Masato Morishige (FC
Tokyo), Yasuyuki Konno (Gamba Osaka), Yuto Nagatomo (Inter Milan), Maya
Yoshida (Southampton), Masahiko Inoha (Jubilo Iwata), Atsuto Uchida
(Schalke 04), Hiroki Sakai (Hannover 96), Gotoku Sakai (VfB Stuttgart).
Viungo: Yasuhito Endo (Gamba
Osaka), Keisuke Honda (AC Milan), Shinji Kagawa (Manchester United),
Makoto Hasebe (FC Nuremberg), Hiroshi Kiyotake (FC Nuremberg), Hotaru
Yamaguchi (Cerezo Osaka), Toshihiro Aoyama (Sanfrecce Hiroshima), Manabu
Saito (Yokohama F. Marinos).
Washambuliaji: Shinji Okazaki
(Mainz), Yoichiro Kakitani (Cerezo Osaka), Yuya Osako (TSV Munich 1860),
Yoshito Okubo (Kawasaki Frontale).
Kundi D
Uruguay
Uruguay
imewaita wachezaji 23 wakiwemo wachezaji wa Liverpool Luis Suarez na
Sebastian Coates. Mshambuliaji wa Paris St-Germain Edinson Cavani na
Diego Forlan, 34, anayekipiga nchini Japan, pia wameitwa.
Kikosi kamili:
Walinda mlango: Fernando Muslera (Galatasaray), Martin Silva (Vasco da Gama), Rodrigo Munoz (Libertad).
Walinzi: Maximiliano Pereira
(Benfica), Diego Lugano (West Bromwich Albion), Diego Godin, Jose Maria
Gimenez (both Atletico Madrid), Sebastian Coates (Liverpool), Martin
Caceres (Juventus), Jorge Fucile (Porto).
Viungo: Alvaro Gonzalez
(Lazio), Alvaro Pereira (Sao Paulo), Walter Gargano (Parma), Egidio
Arevalo Rios (Morelia), Diego Perez (Bologna), Cristian Rodriguez
(Atletico Madrid), Gaston Ramirez (Southampton), Nicolas Lodeiro
(Botafogo).
Washambuliaji: Luis Suarez
(Liverpool), Edinson Cavani (Paris St-Germain), Abel Hernandez
(Palermo), Diego Forlan (Cerezo Osaka), Christian Stuani (Espanyol).
Costa Rica
Costa Rica itakwenda nchini
Brazil bila fowadi wake mashuhuri Alvaro Saborio, ambaye amevunjika mguu
wakati wa mazoezi. Joel Campbell, aliyeko Olympiakos kwa mkopo akitokea
Arsenal, na mchezaji wa Fulham Bryan Ruiz, aliyeko kwa mkopo PSV,
wanatengeneza kikosi cha wachezaji 23. Mlinzi wa Everton Bryan Oviedo
atakosekana kutokana na kuugua.
Kikosi kamili:
Walinda mlango: Keylor Navas (Levante), Patrick Pemberton (Alajuelense) Daniel Cambronero (Herediano).
Walinzi: Johnny Acosta
(Alajuelense), Giancarlo Gonzalez (Columbus Crew), Michael Umana
(Saprissa), Oscar Duarte (Bruges), Waylon Francis (Columbus Crew),
Heiner Mora (Saprissa), Junior Diaz (Mainz 05), Christian Gamboa
(Rosenborg), Roy Miller (New York Red Bulls).
Viungo: Celso Borges (AIK),
Christian Bolanos (Copenhagen), Esteban Granados (Herediano), Michael
Barrantes (Aalesund), Yeltsin Tejeda (Saprissa), Diego Calvo
(Valerenga), Jose Miguel Cubero (Herediano).
Washambuliaji: Bryan Ruiz (PSV
Eindhoven, kwa mkopo kutoka Fulham), Joel Campbell (Olympiakos, kwa
mkopo kutoka Arsenal), Randall Brenes (Cartagines), Marco Urena (FC
Kuban Krasnodar).
England
Boss wa England Roy Hodgson
amekitaja kikosi chake cha wachezaji 23 huku wachezaji kadhaa wakikosa
uzoefu wa mashindano ya kimataifa. Wachezaji watatu wa Southampton Luke
Shaw, Adam Lallana na Rickie Lambert na kiungo wa Everton Ross Barkley
wamejumuishwa. Beki wa kulia Ashley Cole, aliyeichezea England michezo
107 hatokuwepo Brazil baada ya kuwachwa kikosini.
Kikosi kamili:
Walinda mlang: Fraser Forster (Celtic), Ben Foster (West Bromwich Albion), Joe Hart (Manchester City).
Walinzi: Leighton Baines
(Everton), Gary Cahill (Chelsea), Phil Jagielka (Everton), Glen Johnson
(Liverpool), Phil Jones (Manchester United), Luke Shaw (Southampton),
Chris Smalling (Manchester United).
Viungo: Ross Barkley
(Everton), Steven Gerrard, Jordan Henderson (both Liverpool), Adam
Lallana (Southampton), Frank Lampard (Chelsea), James Milner (Manchester
City), Alex Oxlade-Chamberlain (Arsenal), Raheem Sterling (Liverpool),
Jack Wilshere (Arsenal).
Washambuliaji: Rickie Lambert
(Southampton), Wayne Rooney (Manchester United), Daniel Sturridge
(Liverpool), Danny Welbeck (Manchester United).
Italia
Mshambuliaji wa Fiorentina
Giuseppe Rossi amewachwa kwenye kikosi cha wachezaji 23, licha ya kupona
goti, lakini Antonio Cassano wa Parma amejumuishwa kikosini baada ya
kupunguza uzito wa kilo 10. Mchezaji wa Torino Ciro Immobile
amejumuishwa baada ya kufunga mabao 22 kwenye Serie A msimu huu.
Kikosi kamili:
Walinda mlango: Gianluigi Buffon (Juventus), Salvatore Sirigu (Paris St Germain), Mattia Perin (Genoa).
Walinzi: Andrea Barzagli,
Leonardo Bonucci, Giorigo Chiellini (wote Juventus), Gabriel Paletta
(Parma), Ignazio Abate, Mattia De Sciglio (wote AC Milan), Matteo
Darmian (Torino).
Viungo: Andrea Pirlo, Claudio
Marchisio (wote Juventus), Thiago Motta, Marco Verratti (both Paris St
Germain), Daniele De Rossi (AS Roma), Antonio Candreva (Lazio), Marco
Parolo (Parma), Alberto Aquilani (Fiorentina).
Washambuliaji: Mario Balotelli
(AC Milan), Antonio Cassano (Parma), Alessio Cerci (Torino), Ciro
Immobile (Torino), Lorenzo Insigne (Napoli).
Kundi E
Switzerland
Kocha wa Switzerland Ottmar
Hitzfeld ametaja kikosi cha wachezaji 23 akiwajumuisha beki wa kulia wa
Juventus Stephan Lichtsteiner na winga wa Bayern Munich Xherdan Shaqiri
wachezaji wenye majina makubwa zaidi kwenye kikosi hicho. Kiungo wa
Fulham Pajtim Kasami amewekwa kwenye orodha ya wachezaji wa dharura.
Kikosi kamili:
Walinda mlango: Diego Benaglio (Wolfsburg), Roman Buerki (Grasshopper), Yann Sommer (Basel).
Walinzi: Johan Djourou
(Hamburg), Michael Lang (Grasshopper), Stephan Lichtsteiner (Juventus),
Ricardo Rodriguez (Wolfsburg), Fabian Schaer (Basel), Philippe Senderos
(Valencia), Steve von Bergen (Young Boys), Reto Ziegler (Sassuolo).
Viungo: Tranquillo Barnetta
(Eintracht Frankfurt), Valon Behrami (Napoli), Blerim Dzemaili (Napoli),
Gelson Fernandes (Freiburg), Gokhan Inler (Napoli), Xherdan Shaqiri
(Bayern Munich), Valentin Stocker (Basel).
Washambuliaji: Josip Drmic
(Nuremberg), Mario Gavranovic (Zurich), Admir Mehmedi (Freiburg), Haris
Seferovic (Real Sociedad), Granit Xhaka (Borussia Monchengladbach).
Wachezaji wa dharura: Marwin
Hitz (Augsburg), Timm Klose (Wolfsburg), Silvan Widmer (Udinese), Eren
Derdiyok (Bayer Leverkusen), Fabian Frei (Basel), Pajtim Kasami
(Fulham), Pirmin Schwegler (Eintracht Frankfurt).
Ecuador
Kiungo wa Manchester United
Antonio Valencia yumo kikosini. Kulikuwa na wachezaji wanne ambao
hawakuwahi kuichezea Ecuador katika kikosi cha maangalizi - kiungo wa
Stuttgart Carlos Gruezo, 19, washambuliaji wa ndani Cristian Penilla,
Angel Mena na Armando Wila lakini ni Gruezo pekee ndiyo amejumuishwa
kwenye kikosi cha mwisho.
Kikosi kamili:
Walinda mlango: Maximo Banguera (Barcelona SC), Alexander Dominguez (LDU Quito), Adrian Bone (El Nacional).
Walinzi: Frickson Erazo
(Flamengo), Jorge Guagua, Oscar Bagui, Gabriel Achilier (all Emelec),
Walter Ayovi (Pachuca), Juan Carlos Paredes (Barcelona SC).
Viungo: Segundo Castillo
(Al-Hilal), Carlos Gruezo (Stuttgart), Renato Ibarra (Vitesse Arnhem),
Cristian Noboa (Dynamo Moscow), Luis Saritama (Barcelona SC), Antonio
Valencia (Manchester United), Edison Mendez (Independiente Santa Fe),
Fidel Martinez (Tijuana), Michael Arroyo (Atlante).
Washambuliaji: Felipe Caicedo
(Al-Jazira), Jefferson Montero (Morelia), Joao Rojas (Cruz Azul), Jaime
Ayovi (Tijuana), Enner Valencia (Pachuca).
Ufaransa
Kiungo
wa Manchester City Samir Nasri amewachwa, wakati boss Didier Deschamps
akisema: "Nimekijenga kikosi bora, Sijawateua wachezaji 23 bora wa
Ufaransa." Kikosi cha Ufaransa kinajumuisha wachezaji tisa wanaokipiga
English; Patrice Evra, Moussa Sissoko na Loic Remy.
Mchezaji wa Bayern Munich Franck Ribery ameondolewa dakika za majeruhi kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya mgongo.
Kikosi kamili:
Walinda mlango: Hugo Lloris (Tottenham Hotspur), Stephane Ruffier (Marseille), Mickael Landreau (Bastia).
Walinzi: Mathieu Debuchy
(Newcastle), Lucas Digne (Paris St-Germain) Patrice Evra (Manchester
United), Laurent Koscielny, Bacary Sagna (both Arsenal), Eliaquim
Mangala (Porto), Mamadou Sakho (Liverpool), Raphael Varane (Real
Madrid).
Viungo: Yohan Cabaye, Blaise
Matuidi (wote Paris St-Germain), Rio Mavuba (Lille), Paul Pogba
(Juventus), Morgan Schneiderlin (Southampton), Moussa Sissoko
(Newcastle), Mathieu Valbuena (Marseille).
Washambuliaji: Karim Benzema
(Real Madrid), Remy Cabella (Montpellier), Olivier Giroud (Arsenal),
Antoine Griezmann (Real Sociedad), Loic Remy (Newastle, kwa mkopo kutoka
QPR).
Honduras
Honduras imewaita wachezaji
sita wanaokipiga kwenye soka la British katika kikosi chake cha
wachezaji 23. Mlinzi wa Hull Maynor Figueroa, kiungo wa Stoke Wilson
Palacios, wachezaji wawili wa Wigan Roger Espinoza na Juan Carlos
Garcia, mchezaji wa Celtic Emilio Izaguirre na mchezaji wa Rangers
Arnold Peralta wote wameitwa.
Kikosi kamili:
Walinda mlango: Noel Valladares, Donis Escober (both Olimpia), Luis Lopez (Real Espana).
Walinzi: Brayan Beckeles
(Olimpia), Emilio Izaguirre (Celtic), Juan Carlos Garcia (Wigan), Maynor
Figueroa (Hull), Victor Bernardez (San Jose Earthquakes), Osman Chavez
(Qingdao Janoon), Juan Pablo Montes (Motagua).
Viungo: Arnold Peralta
(Rangers), Luis Garrido (Olimpia), Roger Espinoza (Wigan), Jorge Claros
(Motagua), Wilson Palacios (Stoke), Oscar Garcia (Houston Dynamo), Andy
Najar (Anderlecht), Mario Martinez (Real Espana), Marvin Chavez (Chivas
USA).
Washambuliaji: Jerry Bengtson
(New England Revolution), Jerry Palacios (Alajuelense), Carlo Costly
(Real Espana), Rony Martinez (Real Sociedad).
Kundi F
Argentina
Mshambuliaji
wa Juventus Carlos Tevez, kama ilivyotarajiwa, hakujumuishwa kwenye
kikosi cha Argentina. Mlinzi wa Manchester City Martin Demichelis na
mchezaji wa Werder Bremen Franco Di Santo walijumuishwa awali kwenye
kikosi cha maangalizi cha wachezaji 30, lakini Di Santo akatemwa baada
ya kikosi kupunguzwa hadi wachezaji 26.
Kikosi kamili:
Walinda mlango: Sergio Romero (Sampdoria), Mariano Andujar (Catania), Agustin Orion (Boca Juniors).
Walinzi: Pablo Zabaleta
(Manchester City), Federico Fernandez (Napoli), Ezequiel Garay
(Benfica), Marcos Rojo (Sporting Lisbon), Hugo Campagnaro (Inter Milan),
Martin Demichelis (Manchester City), Jose Basanta (Monterrey), Nicolas
Otamendi (Atletico Mineiro).
Viungo: Javier Mascherano
(Barcelona), Fernando Gago (Boca Juniors), Lucas Biglia (Lazio), Ever
Banega (Newell's Old Boys), Ricardo Alvarez (Inter Milan), Augusto
Fernandez (Celta Vigo), Jose Sosa (Atletico Madrid), Angel Di Maria
(Real Madrid), Maxi Rodriguez (Newell's Old Boys), Enzo Perez (Benfica).
Washambuliaji: Lionel Messi
(Barcelona), Gonzalo Higuain (Napoli), Sergio Aguero (Manchester City),
Rodrigo Palacio (Inter Milan), Ezequiel Lavezzi (Paris St-Germain).
Bosnia-Hercegovina
Bosnia-Hercegovina awali
kilitaja wachezaji 24 katika kikosi chake cha maangalizi kwa ajili ya
mashindano yao ya kwanza. Mshambuliaji wa Manchester City Edin Dzeko na
mlinda mlango wa Stoke City Asmir Begovic ni wachezaji wawili pekee wa
Premier League kujumuishwa kwenye kikosi hicho.
Kikosi kamili:
Walinda mlango: Asmir Begovic (Stoke City), Asmir Avdukic (Borac Banja Luka), Jasmin Fejzic (VFR Aalen).
Walinzi: Emir Spahic (Bayer
Leverkusen), Toni Sunjic (Zorya Lugansk), Sead Kolasinac (Schalke),
Ognjen Vranjes (Elazigspor), Ervin Zukanovic (Gent), Ermin Bicakcic
(Eintracht Braunschweig), Muhamed Besic (Ferencvaros).
Viungo: Miralem Pjanic (Roma),
Izet Hajrovic (Galatasaray), Mensur Mujdza (Freiburg), Haris Medunjanin
(Gaziantepspor), Senad Lulic (Lazio), Anel Hadzic (Sturm), Tino Susic
(Hajduk), Sejad Salihovic (Hoffenheim), Zvjezdan Misimovic (Guizhour
Renhe), Senijad Ibricic (Erciyesspor), Avdija Vrsaljevic (Hajduk).
Washambuliaji: Vedad Ibisevic (VfB Stuttgart), Edin Dzeko (Manchester City), Edin Visca (Istanbul BB).
Iran
Iran imewaita kikosini kiungo
wa Fulham Ashkan Dejagah na mchezaji wa Charlton Reza Ghoochannejhad.
Boss Carlos Queiroz alimjumuisha katika kikosi cha maangalizi mchezaji
kinda wa Rubin Kazan ambaye hajawahi kuichezea nchi yake Sardar Azmoun
lakini hakumuita kwenye kikosi cha mwisho.
Kikosi kamili:
Walinda mlango: Daniel Davari
(Eintracht Braunschweig), Alireza Haghighi (Sporting Covilha, on loan
from Rubin Kazan), Rahman Ahmadi (Sepahan).
Walinzi: Hossein Mahini
(Persepolis), Steven Beitashour (Vancouver Whitecaps), Pejman Montazeri
(Umm Salal), Jalal Hosseini (Persepolis), Amir-Hossein Sadeghi
(Esteghlal), Ahmad Alenemeh (Naft), Hashem Beikzadeh (Esteghlal),
Mehrdad Pouladi (Persepolis).
Viungo: Javad Nekounam (Kuwait
SC), Andranik Teymourian (Esteghlal), Reza Haghighi (Persepolis),
Ghasem Haddadifar (Zob Ahan), Bakhtiar Rahmani (Foolad), Ehsan Hajsafi
(Sepahan).
Washambuliaji: Ashkan Dejagah
(Fulham), Masoud Shojaei (Las Palmas), Alireza Jahanbakhsh (NEC
Nijmegen), Reza Ghoochannejhad (Charlton), Karim Ansarifard (Tractor
Saz, on loan from Persepolis), Khosro Heydari (Esteghlal).
Nigeria
Nigeria ilimtaja kwenye kikosi
chake cha maangalizi mshambuliaji wa Newcastle Shola Ameobi. Wachezaji
wenza wa Premier League Peter Odemwingie, Victor Moses, Joseph Yobo na
John Mikel Obi pia wameitwa kikosini.
Kikosi kamili:
Walinda mlango: Vincent Enyeama (Lille), Austin Ejide (Hapoel Be'er Sheva), Chigozie Agbim (Gombe United).
Walinzi: Elderson Echiejile
(Monaco), Efe Ambrose (Celtic), Godfrey Oboabona (Rizespor), Azubuike
Egwuekwe (Warri Wolves), Kenneth Omeruo (Middlesbrough), Juwon Oshaniwa
(Ashdod), Joseph Yobo (Norwich, on loan from Fenerbahce), Kunle Odunlami
(Sunshine Stars).
Viungo: John Mikel Obi
(Chelsea), Ramon Azeez (Almeria), Ogenyi Onazi (Lazio), Reuben Gabriel
(Waasland-Beveren), Michael Babatunde (Volyn Lutsk).
Washambuliaji: Ahmed Musa
(CSKA Moscow), Shola Ameobi (Newcastle), Emmanuel Emenike (Fenerbahce),
Michael Uchebo (Cercle Brugge), Peter Odemwingie (Stoke), Victor Moses
(Liverpool, kwa mkopo akitokea Chelsea), Uche Nwofor (Heerenveen).
Kundi G
Ujerumani
Ujerumani
imemuita kikosini mtaalamu wao wa Kombe la Dunia Miroslav Klose ambaye
anahitaji magoli mawili tu kuivunja rekodi ya Ronaldo anayeshikilia
rekodi ya ufungaji bora wa Kombe la Dunia kwa magoli yake 15. Kiungo wa
Real Madrid Sami Khedira amejumuishwa pia licha kuwa nje karibu nusu ya
msimu kufuatia kufanyiwa upasuaji.
Kikosi kamili:
Walinda mlango: Manuel Neuer (Bayern Munich), Roman Weidenfeller (Borussia Dortmund), Ron-Robert Zieler (Hannover)
Walinzi: Jerome Boateng
(Bayern Munich), Erik Durm (Borussia Dortmund), Kevin Grosskreutz
(Borussia Dortmund), Benedikt Howedes (Schalke), Mats Hummels (Borussia
Dortmund), Philipp Lahm (Bayern Munich), Per Mertesacker (Arsenal).
Viungo: Julian Draxler
(Schalke), Matthias Ginter (Freiburg), Mario Gotze (Bayern Munich),
Christoph Kramer (Borussia Monchengladbach), Sami Khedira (Real Madrid),
Toni Kroos (Bayern Munich), Thomas Muller (Bayern Munich), Mesut Ozil
(Arsenal), (Borussia Dortmund), Andre Schurrle (Chelsea), Bastian
Schweinsteiger (Bayern Munich).
Washambuliaji: Miroslav Klose (Lazio), Lukas Podolski (Arsenal).
Ureno
Nahodha wa Ureno Cristiano
Ronaldo ametajwa kwenye kikosi cha wachezaji 23 kwa ajili ya Kombe la
Dunia licha ya kukumbwa na majeruhi siku za hivi karibuni. Winga wa
Manchester United ni mchezaji pekee kutoka Premier League kujumuishwa
kikosini. Winga wa FC Porto Ricardo Quaresma alikuwa mchezaji pekee
mwenye jina kubwa kuondolewa kwenye kikosi cha Paulo Bento.
Kikosi kamili:
Walinda mlango: Beto (Sevilla), Eduardo (Braga), Rui Patricio (Sporting).
Walinzi: Andre Almeida
(Benfica), Bruno Alves (Fenerbahce), Fabio Coentreo (Real Madrid), Joao
Pereira (Valencia), Neto (Zenit), Pepe (Real Madrid), Ricardo Costa
(Valencia).
Viungo: Joao Moutinho
(Monaco), Miguel Veloso (Dinamo Kiev), Raul Meireles (Fenerbahce), Ruben
Amorim (Benfica), William Carvalho (Sporting).
Washambuliaji: Cristiano
Ronaldo (Real Madrid), Eder (SC Braga), Helder Postiga (Lazio), Hugo
Almeida (Besiktas), Nani (Manchester United), Rafa (Braga), Varela (FC
Porto), Vieirinha (Wolfsburg).
Ghana
Mlinzi wa Leicester Jeffrey
Schlupp ni miongoni mwa wachezaji watatu waliotemwa kwenye kikosi cha
Ghana kutoka wachezaji 26 wa maangalizi hadi 23 watakaoiwakilisha nchi
hiyo nchi Brazil. Mshambuliaji wa Helsingborgs David Accam na Jerry
Akaminko anayekipiga nchini Uturuki, ambaye alivunjika mfupa katika
mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Uholanzi, wanakosekana lakini
kiungo wa zamani wa Chelsea Michael Essien ametajwa kikosini.
Kikosi kamili:
Walinda mlango: Fatau Dauda (Orlando Pirates), Adam Kwarasey (Stromsgodset), Stephen Adams (Aduana Stars).
Walinzi: Samuel Inkoom
(Platanias), Daniel Opare (Standard Liege), Harrison Afful (Esperance),
John Boye (Rennes), Jonathan Mensah (Evian), Rashid Sumalia (Mamelodi
Sundowns).
Viungo: Michael Essien (AC
Milan), Sulley Muntari (AC Milan), Rabiu Mohammed (Kuban Krasnodar),
Kwadwo Asamoah (Juventus), Emmanuel Agyemang-Badu (Udinese), Afriyie
Acquah (Parma), Christian Atsu (Vitesse), Albert Adomah (Middlesbrough),
Andre Ayew (Marseille), Mubarak Wakaso (Rubin Kazan).
Washambuliaji: Asamoah Gyan
(Al Ain), Kevin-Prince Boateng (Schalke 04), Abdul Majeed Waris
(Valenciennes), Jordan Ayew (Sochaux).
Marekani
Kocha wa Marekani Jurgen
Klinsmann aliwataja wachezaji wanne wa Premier League, wakiwepo walinda
mlango wawili katika kikosi chake cha wachezaji 23. Brad Guzan na Tim
Howard wamejumuishwa, pamoja na mlinzi Geoff Cameron na mshambuliaji
Jozy Altidore. Landon Donovan alitajwa kwenye kikosi cha maangalizi cha
wachezaji 30, lakini ameondolewa kwenye kikosi cha wachezaji 23 licha
kufunga magoli 57 katika michezo 155 ya nchi yake.
Kikosi kamili:
Walinda mlango: Brad Guzan (Aston Villa), Tim Howard (Everton), Nick Rimando (Real Salt Lake).
Walinzi: DaMarcus Beasley
(Puebla), Matt Besler (Sporting Kansas City), John Brooks (Hertha
Berlin), Geoff Cameron (Stoke City), Timmy Chandler (Nuremberg), Omar
Gonzalez (LA Galaxy), Fabian Johnson (Hoffenheim), DeAndre Yedlin
(Seattle Sounders).
Viungo: Kyle Beckerman (Real
Salt Lake), Alejandro Bedoya (Nantes), Michael Bradley (Toronto FC),
Brad Davis (Houston Dynamo), Mix Diskerud (Rosenborg), Julian Green
(Bayern Munich), Jermaine Jones (Besiktas), Graham Zusi (Sporting Kansas
City).
Washambuliaji: Jozy Altidore
(Sunderland), Clint Dempsey (Seattle Sounders), Aron Johannsson (AZ
Alkmaar), Chris Wondolowski (San Jose Earthquakes).
Kundi H
Ubelgiji
Ubelgiji
amewaita wachezaji 12 wanaokipiga Premier League katika kikosi chake
ikimjumuisha kwa mara ya kwanza winga wa Manchester United Adnan
Januzaj. Chelsea imewatoa Eden Hazard, Romelu Lukaku na Thibaut
Courtois, wakati Arsenal ina Thomas Vermaelen na Tottenham ina Jan
Vertonghen, Mousa Dembele na Nacer Chadli. Hawa wote wanakwenda Brazil.
Sammy Bossut aliitwa baada ya mchezaji wa Anderlecht Silvio Proto
kuvunjika mkono katika wiki ya mwisho ya msimu wa ligi ya Ubelgiji.
Kikosi kamili:
Walinda
mlango: Thibaut Courtois (Atletico Madrid, kwa mkopo akitokea Chelsea),
Simon Mignolet (Liverpool), Koen Casteels (Hoffenheim), Sammy Bossut
(Zulte Waregem).
Walinzi: Toby Alderweireld
(Atletico Madrid), Laurent Ciman (Standard Liege), Nicolas Lombaerts
(Zenit St Petersburg), Vincent Kompany (Manchester City), Daniel van
Buyten (Bayern Munich), Anthony Vanden Borre (Anderlecht), Thomas
Vermaelen (Arsenal), Jan Vertonghen (Tottenham).
Viungo: Nacer Chadli, Mousa
Dembele (both Tottenham), Steven Defour (Porto), Kevin de Bruyne
(Wolfsburg), Marouane Fellaini, Adnan Januzaj (wote Manchester United),
Eden Hazard (Chelsea), Kevin Mirallas (Everton), Divock Origi (Lille),
Axel Witsel (Zenit St Petersburg).
Washambuliaji: Romelu Lukaku (Everton, kwa mkopo akitokea Chelsea), Dries Mertens (Napoli).
Algeria
Mchezaji kinfa wa Tottenham
Nabil Bentaleb yumo kwenye kikosi cha wachezaji 23 wa Algeria kwa ajili
ya Kombe la Dunia. Kiungo wa Inter Milan Saphir Taider pia ameteuliwa
lakini mchezaji wa Crystal Palace Adlene Guedioura aliondolewa kwenye
kikosi cha maangalizi.
Kikosi kamili:
Walinda mlango: Rais Mbolhi (CSKA Sofia), Cedric Si Mohamed (CS Constantine), Mohamed Lamine Zemmamouche (USM Alger).
Walinzi: Essaid Belkalem
(Watford, on loan from Granada), Madjid Bougherra (Lekhwya Club),
Liassine Cadamuro (Mallorca), Faouzi Ghoualm (Napoli), Rafik Halliche
(Academica Coimbra), Aissa Mandi (Stade Reims), Carl Medjani
(Valenciennes), Djamel Mesbah (Livorno), Mehdi Mostefa (AC Ajaccio).
Viungo: Nabil Bentaleb
(Tottenham), Yasine Brahimi (Granada), Medhi Lacen (Getafe), Saphir
Taider (Inter Milan), Hassan Yebda (Udinese).
Washambuliaji: Abdelmoumene
Djabou (Club Africain), Sofiane Feghouli (Valencia), Nabil Ghilas
(Porto), Riyad Mahrez (Leicester City), Islam Slimani (Sporting Lisbon,
Portugal), Hilal Soudani (Dinamo Zagreb).
Urusi
Boss wa Urusi Fabio Capello
ametaja wachezaji wanaocheza ligi ya ndani katika kikosi chake cha
wachezaji 23. Mshambuliaji wa Reading Pavel Pogrebnyak aliondolewa
kwenye kikosi cha maangalizi cha wachezeji 30 ambacho wachezaji wa
zamani wa Premier League Andrey Arshavin, Roman Pavlyuchenko na Diniyar
Bilyaletdinov hakujumuishwa.
Kikosi kamili:
Walinda mlango: Igor Akinfeev (CSKA Moscow), Yury Lodygin (Zenit St Petersburg), Sergey Ryzhikov (Rubin Kazan).
Walinzi: Vasili Berezutskiy
(CSKA Moscow), Vladimir Granat (Dynamo Moscow), Andrey Eshchenko (Anzhi
Makhachkala), Sergey Ignashevich (CSKA Moscow), Alexey Kozlov (Dynamo
Moscow), Dmitry Kombarov (Spartak Moscow), Andrey Semenov (Terek
Grozny), Georgi Schennikov (CSKA Moscow).
Viungo: Denis Glushakov
(Spartak Moscow), Igor Denisov (Dynamo Moscow), Alan Dzagoev (CSKA
Moscow), Yury Zhirkov (Dynamo Moscow), Alexey Ionov (Dynamo Moscow),
Alexander Samedov (Lokomotiv Moscow), Victor Faizulin (Zenit St
Petersburg), Oleg Shatov (Zenit St Petersburg), Roman Shirokov
(Krasnodar).
Washambuliaji: Maxim Kanunnikov (Amkar Perm), Alexander Kerzhakov (Zenit St Petersburg), Alexander Kokorin (Dynamo Moscow).
Korea Kusini
Korea Kusini imekitaja kikosi
chake cha wachezaji 23 ikiwajumuisha wachezaji watano wanaokipiga kwenye
soka la English. Wachezaji wa Cardiff City Kim Bo-kyong, Ki Sung-yeung,
aliyepelekwa kwa mkopo Sunderland akitokea Swansea, na mshambuliaji wa
Arsenal Park Chu-young wameitwa. Mchazaji wa Bolton Lee Chung-yong na
mchezaji wa QPR Yun Suk-young pia wanakwenda Brazil.
Beki wa kushoto chaguo la
kwanza Kim Jin-soo alilazimishwa kutemwa kikosini kwa sababu ya majeruhi
ya enka na nafasi yake ikatwaliwa na mlinzi anayekipiga Ujerumani Park
Joo-ho.
Kikosi kamili:
Walinda mlango: Jung Sung-ryeong (Suwon Bluewings), Kim Seung-gyu (Ulsan Horang-i), Lee Bum-young (Busan I'Park)
Walinzi: Yun Suk-young (QPR),
Kim Young-kwon (Guangzhou Evergrande), Hwang Seok-ho (Sanfrecce
Hiroshima), Hong Jeong-ho (Augsburg), Kwak Tae-hwi (Al Hilal), Lee Yong
(Ulsan Horang-i), Kim Chang-soo (Kashiwa Reysol), Park Joo-ho (Mainz)
Viungo: Ki Seung-yueng
(Sunderland, kwa mkopo akitokea Swansea), Ha Dae-sung (Beijing Guoan),
Han Kook-young (Kashiwa Reysol), Park Jung-woo (Guangzhou R&F), Son
Heung-min (Bayer Leverkusen), Kim Bo-kyung (Cardiff City), Lee
Chung-yong (Bolton Wanderers), Ji Dong-won (Augsburg).
Washambuliaji: Koo Ja-cheol (Mainz), Lee Keun-ho (Sangju Sangmu), Park Chu-young (Arsenal), Kim Shin-wook (Ulsan Horang-i).