SAFARI YA RAGE KUTOWEKA SIMBA SC YAIVA....SERIKALI YAPITISHA KATIBA, MCHAKATO WA UCHAGUZI KUANZA
https://samchardtz.blogspot.com/2014/05/safari-ya-rage-kutoweka-simba-sc.html
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
KATIBA
ya Wekundu wa msimbazi Simba sc imekamilika baada ya kufanyiwa
marekebisho na kukabidhi kwa uongozi wa klabu hiyo chini ya mwenyekiti
Ismail Aden Rage.
Katibu
mkuu wa Simba sc, Ezekiel Kamwaga amezungumza na waandishi wa habari
leo hii na kueleza kuwa tayari wameshakabidhiwa katiba yao kutoka
serikalini na kinachofuata na kuanza kwa mchakato wa uchaguzi .
Awali uchaguzi wa Simba ulitakiwa kufanyika wiki iliyopita, lakini kutokamilika kwa katiba kulikwamisha mchakato mzima.
Kamwaga
alisema baada ya zoezi la katiba kukamilika, kesho wanatarajia kukutana
na kamati ya uchaguzi chini ya mwenyikiti wake, Mwanasheria Dkt. Damas
Ndumbaro ili kupanga mchakato mzima.
Katibu huyo aliongeza kuwa baada ya kamati kukutana, taratibu zote zitawekwa wazi na wenye nia ya kugombea wataanza rasmi mchakato.
Aidha,
Kamwaga alisema kuwa katiba yao imepitisha kuwepo kwa Kamati ya Maadili
na Rufaa ambazo Mwenyekiti wa Simba SC, Ismail Aden Rage atazitangaza
juma lijalo.
Pia katiba imependekeza kuwepo kwa mgombea mmoja mwanamke wa kuchaguliwa.
Kamwaga alisema, vipengele vyote vimepita katika katiba yao, isipokuwa cha ibara ya 26(4) kuhusu sifa za mgombea.
“Katiba ya sasa ni lazima katika wagombea watano wa kamati ya utendaji nafasi moja awepo mwanamke”.
“Nawaomba wanawake wanaojiona kuwa na sifa wajitokeze kwa wingi kuwania uongozi”.
“Wanaweza hata wakiwa watatu, lakini nafasi moja ni lazima,”alifafanua
Kamwag