LIVERPOOL KYATOKA 3-3 NA CRYSTAL PALACE
https://samchardtz.blogspot.com/2014/05/liverpool-kyatoka-3-3-na-crystal-palace.html
Kazini: Mfungaji wa bao la kwanza la Liverpool, Joe Allen (kushoto) akichuana na mshambuliaji wa Palace, Marouane Chamakh
Ajabu: Gayle akishangilia na Yannick Bolasie, baada ya kuchafua hali ya hewa kwa Liverpool uwanja wa Selhurst Park
Manyoya
tu: Kipa wa Palace, Julian Speroni akishindwa kuokoa mpira uliopigwa na
Daniel Sturridge na kuifungia Liverpool bao la pili.
NDOTO
za majogoo wa jiji, klabu ya Liverpool kufuta ukame wa miaka 24 bila
kikombe zimeanza kufifia baada ya usiku huu kutoka sare ya mabao 3-3
dhidi ya wenyeji Crystal Palace katika mchezo wa ligi kuu soka nchini
England.
Kwa
matokeo ya mchezo huo, Liverpool wanapanda kileleni baada ya kufikisha
pointi 81, huku Manchester City wenye michezo miwili mkononi wakiwa
nafasi ya pili kwa pointi 80.
Majogoo
wa jiji walikuwa wa kwanza kuandika bao la kuongoza dakika ya 18
kipindi cha kwanza kupitia kwa Joe Allen, baadaye dakika ya 53, Daniel
Sturridge akifunga bao la pili, huku bao la tatu likifungwa dakika ya 55
kupitia kwa Luis Suarez.
Wakati Liverpool wakiamini watashinda mechi ya leo, kibao kilibadilika dakika ya 79 baada ya Damien Delaney kusawazisha bao la kwanza.
Ikiwa kama utani vile, dakika ya 81 Dwight Gayle aliisawazishia Palace bao la pili.
Liverpool wakazidi kuchanganyikiwa na kuona dakika haziendi. Mnamo dakika ya 88 Dwight Gayle aliandika bao la tatu na mechi kuisha kwa sare ya 3-3.
Baada
ya kipyenga cha mwisho kupulizwa, Luis Suarez aliangua kilio kikubwa
kwa kuamini kuwa kuna asilimia kubwa wameshaweka reheni mbio zao za
ubingwa.
Liverpool
wamebakiwa na mechi moja mkononi ambayo wakishinda watafikisha pointi
84, wakati Man city wakishinda mechi zao mbili watafikisha pointi 86 na
kutwaa taji.
Kama
Man City watashinda mechi moja na kufungwa moja, halafu Liverpool
wakashinda mechi ya mwisho, basi majogoo hao wa jiji watafanikiwa kutwaa
ubingwa.
Liverpool wanategemea muujiza wa soka kutokea.