SUPERMODEL FLAVIANA MATATA AVISHWA PETE YA UCHUMBA
http://samchardtz.blogspot.com/2014/11/supermodel-flaviana-matata-avishwa-pete.html
Post
hii ya leo ni maalum kwa ajili ya Mwanamitindo wa kimataifa anaetokea
Tanzania Flaviana Matata ambae amekua akiishi Marekani, kafungua page
mpya kwenye maisha yake baada ya kuvishwa pete ya Uchumba.
Kwa furaha aliyokua nayo, Flavvy aliipost picha kwenye page yake ya Instagram@FlavianaMatata Nov 16 2014 na kuionyesha hiyo pete na kama vile haitoshi, akaandika maneno ya ‘I said YES‘ ambapo Yes aliiandika kwa herufi kubwa…. yaani ‘Nilikubali au nilisema ndio’
Baada ya kujua kwamba sasa Flaviana Matata kavishwa pete tayari, kingine kinachosubiriwa ni kumjua shemeji.

.
Sifa
mojawapo ya Flaviana Matata ni pamoja na kuingia kwenye list ya
MillardAyo ya mastaa ambao ni Watanzania na wanaishi nje ya nchi lakini
wamekua wakiikumbuka nchi yao na hurudi mara kwa mara kwa ajili ya kazi
za kusaidia jamii walizozianzisha.
Headlines za Flavvy mara nyingi zimekua za kazi ya msaada anaoutoa mashuleni au kwa Wanafunzi kupitia Flaviana Matata Foundation.

