SANGOMA AZIMIA AKITOA MAJINI SHULENI!
INASHANGAZA sana! Katika hali isiyokuwa ya kawaida mganga wa kienyeji ‘sangoma’ mmoja aliyefahamika kwa jina la Lambalamba amejikuta aki...
http://samchardtz.blogspot.com/2014/11/sangoma-azimia-akitoa-majini-shuleni.html
INASHANGAZA sana! Katika hali isiyokuwa ya kawaida mganga wa kienyeji ‘sangoma’ mmoja aliyefahamika kwa jina la Lambalamba amejikuta akiingia kwenye hatua ya nusu kifo kufuatia kupoteza fahamu baada ya kuelemewa na majini aliyokuwa akiyatoa shuleni.

Tukio
hilo la aina yake lilijiri hivi karibuni maeneo ya Kiluvya - Madukani
jijini Dar es Salaam kwenye Shule ya Msingi Makurunge ambapo sangoma
huyo aliitwa kuyatoa majini yaliyokuwa yakiwafanyia mauzauza wanafunzi
na walimu.
ILIVYOKUWA
Kwa
mujibu wa shuhuda mmoja wa tukio hilo, wanafunzi wa shule hiyo wamekuwa
wakisikia sauti za ajabuajabu shuleni hapo hali iliyokuwa ikiwafanya
wasome kwa hofu. “Hali hiyo ilipozidi baadhi ya wanafunzi wakaenda
kuwaambia wazazi wao ambao nao walipopeleleza kwa baadhi ya walimu
walihakikishiwa kwamba ni kweli shuleni hapo kuna majini yanawasumbua
wanafunzi na walimu pia,” alisema shuhuda huyo.
Timu hiyo ya ‘Sangoma’ ikimwamtoa mbuzi kafara kwa ajili ya zoezi hilo.
Ili
kuwanusuru wanafunzi kutoka kwenye mauzauza hayo, wazazi waliweka kikao
cha dharura na kuamua kuandika barua kwenye ofisi za serikali ya mtaa
ili kuomba kibali cha kuitwa sangoma mkali, mwenye sifa, anayejua
majini, afike shuleni hapo kuyafukuza.
Ilidaiwa
kuwa mauzauza ya shuleni hapo ni wanafunzi wakienda chooni husikia
vilio vya watoto wachanga au paka lakini hawaonekani. Wakati mwimgine
hupatwa na hali isiyoweza kuelezewa kwa lugha sahihi.
‘Sangoma’ hao wakimsaidia mmoja wao aliyezidiwa na nguvu za majini.
SANGOMA ATINGA
Ikazidi
kudaiwa kuwa, serikali ya mtaa japokuwa haiamini ushirikina,
iliwaruhusu wazazi hao kutekeleza azma yao lakini serikali isihusike kwa
lolote litakalotokea. Siku ilifika, sangoma huyo akaitwa, akiwa na
wasaidizi wake wawili, alitia timu kwenye eneo hilo na kujigamba kuwa,
tabu ya majini imekwisha! Yeye ndiye Lambalamba bwana!
ATAKIWA MBUZI MNONO
Habari
zinasema kuwa, ili kazi ifanyike kwa ufanisi na kuweza kuleta tija na
ili wanafunzi hao wampe tano kwa kazi, sangoma huyo alitaka mbuzi mnono
kwa ajili ya kumchinja ili damu yake imwagikie eneo hilo na majini
kukimbia.
‘Sangoma’ wakiendelea kutoa msaada kwa mwenzao aliyeshambuliwa na majini.
Mbuzi
alifikishwa, maandalizi ya uchinjaji yakafuatia huku sangoma akianza
kusema maneno ya ‘kitaalam’ kuashiria kuwa sasa kazi imeanza, majini
yakae tayari kwa kukimbia eneo la shule.
HALI TETE
Ikazidi
kudaiwa kuwa, wakati sangoma akisemasema maneno yake ya kufukiza,
ghafla alianza kuyumbayumba mpaka kujikuta yupo chini kisha akatulia
tuli licha ya wananchi, wakiwemo wanafunzi kumpigia makofi.

‘Sangoma’ akiwa hoi maada ya kushambuliwa.
WASAIDIZI WAHAHA
Ilibainika
baadaye kwamba, sangoma huyo aliyekuwa amelala chali kama kwenye
msalaba alikuwa amepoteza fahamu hivyo wasaidizi wake walianza kuhaha
kwa kummwagia maji ndoo nzima ili azinduke kama siyo kurejea kwenye uhai
wake (pichani).
CHA AJABU SASA
Cha
ajabu sasa, sangoma akiwa hajitambui chini na wasaidizi wake
wakiendelea kumzindua, msichana mmoja ambaye hakujulikana jina mara
moja, alianza kupagawa, akaishiwa nguvu huku akisemasema maneno
yasiyoeleweka, watu ‘waliokula chumvi nyingi’ wakasema amekumbwa na
majini.

Mmoja ya raia waliokuwa wakishabikia akiwa hoi baada ya kupigwa na majini.
“Huyo
naye ni majini yamemvaa. Huenda yalipokuwa yanatolewa na mganga mengine
yakahamia kwake,” alisema mzee mmoja bila kutaja jina lake. Ilibidi
wasaidizi wa sangoma huyo wahamie kwake ili kumnusuru na janga hilo
ambapo baada ya muda, msichana huyo alirejea katika hali yake ya
kawaida.
HALI YATULIA, ZOEZI LASITISHWA
Baada
ya sangoma naye kuzinduka, zoezi la kuyatoa majini shuleni hapo
lilisimama huku mikakati ikiwekwa kwamba shughuli hiyo itaendelea tena
siku kadhaa mbele.

Baadhi ya raia wakishudia yaliyojiri eneo la tukio.
MWENYEKITI WA MTAA ANENA
Naye
Mwenyekiti wa Mtaa wa Kiluvya-Madukani, Adelaida Bruno alisema yeye
alipelekewa barua ya maombi kutoka kwa wananchi wake wakimtaka awaruhusu
kumuita sangoma kwa ajili ya kuwasaidia kuondoa mambo hayo ya mauzauza
shuleni hapo. “Mimi kama serikali, hatuamini ushirikina, niliipokea hiyo
barua, nikawaambia kama wamekubaliana kumwita sangoma kuwasaidia basi
wafanye wao wenyewe. Na siku hiyo ya sangoma sikuhudhuria,” alisema
mwenyekiti huyo.
MWALIMU MKUU ATUPIA KAMATI
Uwazi
lilimtafuta mwalimu mkuu wa shule hiyo ambaye hakutaka kujitambulisha
jina ambapo alisema siku ya tukio hakuwepo lakini alisikia kutoka kwa
watu na kama ni ukweli utakuwepo kwenye kamati ya shule.
Chanzo Global


