Flatnews

MAREFA 7 WAFUNGIWA TFF


chama

Na Bertgha Lumala, Dar es Salaam
WAKATI Kamati ya Waamuzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kesho inatarajia kutangaza rasmi adhabu ilizozitoa dhidi ya marefa walioboronga katika raundi saba zilizopita za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL), zaidi ya marefa saba wameondolewa katika michuano hiyo.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Saloum Chama, wajumbe wa kamati hiyo wamekutana jijini Dar es Salaam leo kuanzia saa mbili asubuhi pamoja na maofisa wengine wa TFF kutoka Bodi ya Ligi Kuu nchini (TPLB) kupitia mikanda ya mechi iliyorekodiwa na Azam TV walionunua haki za matangazo ya televisheni ya VPL na ripoti za marefa na makamisaa wa mechi zilizopita za VPL na FDL.
“Bado tunaendelea kupitia ripoti na mikanda pamoja na kuwasikiliza maofisa wa TFF waliokwenda kusimamia mechi za Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza. Tumeanza saa mbili asubuhi lakini mpaka sasa (saa 10:32 jioni) bado hatujamaliza, mechi ni nyingi, hovyo ripoti ni nyingi pia,” amesema Chama.
Apoulizwa kama kuna waamuzi waliochukuliwa hatua kwa kuzisigina Sheria 17 za Soka, Chama alisema: “Ndiyo, mpaka sasa marefa saba wameondolewa kwenye ratiba ya kuchezesha mechi kutokana na makosa mbalimbali, siwezi kukutajia majina kwa sababu sijamaliza kazi.”
“Kesho tutangaza rasmi baada ya kukamilisha kazi,” ameongeza kiongozi huyo huku akiweka wazi kwamba kikao hicho kilifanyika kwenye ofisi za TPLB zilizopo Posta jijini Dar es Salaam.
Kufinyangwa kwa Sheria 17 za Soka bado ni tatizo kubwa linalotafuna maendeleo ya soka la Tanzania

Post a Comment

emo-but-icon

item